Rais Kikwete akikabidhi medali ya Dk Chagula

Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi, Clement Chagula na bintiye Olivia Chagula medali kwa niaba ya baba na babu yao Marehemu Dk. Wilbert Chagula, ambaye aikuwa ni mmoja wa mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza na mmoja wa watu maarufu waliotunukiwa nishani katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru. Chagula, ambaye ni mtoto wa marehemu, hakuweza kufika Dar es Salaam kupokea medali …

Jeshi la Marekani laondoka Iraq

WANAJESHI wa mwisho wa Marekani nchini Iraq wameondoka kabla ya siku ya mwisho wa mwaka 2011, ambao ndio muda uliokubaliwa baina ya Iraq na Marekani jeshi hilo kuondoka. Taarifa zaidi kutoka Iraq zinasema gari la jeshi la mwisho lilivuka mpaka na kuingia Kuwait asubuhi mapema leo, na kumaliza vita vya Iraq vya karibu miaka 9. Msafara wa mwisho wa matingatinga …

ICC yasema mauaji ya Gadaffi ni uhalifu

*Yaanza kuwasaka waliohusika wahukumiwe KIFO cha aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ‘kimezua utata’ na kudaiwa kuwa waliohusika kumuua wamefanya uhalifu wa kivita, amesema Kiongozi wa Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa kuhusu kesi za jinai, Luis Moreno-Ocampo. Aidha Moreno-Ocampo amesema ICC imeanza kulishuku Baraza la Mseto la Libya (NTC) kuhusiana na uhalifu huo. Kanali Gaddafi aliuawa tarehe 20 …