Elimu ya juu na changamoto ya ongezeko la gharama

Na Mwandishi Wetu UKUAJI wa kiwango cha elimu hapa nchini kuanzia ngazi ya msingi hadi chuo kikuu umekuwa sio wa kiwango cha kuridhisha, na hii ni kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hii muhimu katika ukombozi wa fikra. Jitihada kadhaa zimekuwa zikifanywa na serikali kupitia Wizara ya Elimu ikiwa ni pamoja na kuongeza, kuboresha miundombinu, kuongeza walimu na kubadilisha mitaala …

Makovu ya Nduli Amini hayata sahaulika- Askofu Kilaini

ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini, amesema makovu yaliyotokea katika vita vya Kagera vilivyoanzishwa na Nduli Idd Amini wa Uganda hayawezi kusahaulika kwa wakatoliki wa Kasambya na hata wana-Kagera wote. Kilaini ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akiwahubiri waumini wa Parokia Kasambya Kyaka na wageni anuai, kwenye Jubilee ya Miaka 75 ya kuanzishwa kwa Parokia hiyo iliyopo …

Kafulila afukuzwa NCCR-Mageuzi

Ampigia magoti Mbatia kwa machozi, wajumbe wakataa kumsamehe CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe. Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Poroin jijini Dar es Salaam …

Mabondia Matumla na Oswald wapima vipimo

Na Mwandishi Wetu MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa, wamepima uzito na kukutwa wapo fiti kiafya. Pambano hilo la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam. Daktari wa mchezo wa ngumi nchini, Charles Kilaga, …

TIA wazindua mkataba wa huduma kwa mteja

Naibu Waziri wa Fedha Pereira Ame Silima (katikati) akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) jana jijini Dar es Salaam mara baada ya mahafali ya tisa (9) ya Taasisi hiyo. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushari ya TIA Profesa Isaya Jairo (kushoto) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TIA Shah Hanzuruni (kulia) Naibu Waziri wa …

Rais Kikwete alipowasili Dar kutokea Uganda

Rais Jakaya Kikwete akiwa na mazungumzo na Makamu wa Rais Dk Mohamed Ghalib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mara baada ya kurejea jijjini Dar es Salaam kutoka Kampala, Uganda, alikohudhuria mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za maziwa makuu. (Picha na Ikulu)