Maafa makubwa Dar, haijawahi tokea; Watu, nyumba zasombwa na mafuriko

Na Joachim Mushi MVUA kubwa imeendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kusababisha maafa makubwa. Taarifa zinaeleza watu zaidi ya nane wanahofiwa kufa na uharibifu mkubwa wa mali za wananchi na miundombinu (madaraja) baada ya mafuriko makubwa kuyakumba maeneo ya mabonde ya Kigogo, Tandale, Tabata na Kiwalani jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi zinasema huenda idadi …

Kabila aapishwa Kinshasa, ulinzi mkali wawekwa

JESHI la Congo (DRC) limesambaza vifaru maeneo yote jijini Kinshasa ikiwa ni hatua ya kujihami na vurugu zozote ambazo zingejitokeza katika hafla ya kuapishwa kwa Rais Joseph Kabila kufuatia Uchaguzi wenye utata uliofanywa mwezi uliopita. Hata hivyo ni viongozi wachache tu wa mataifa ya Afrika wameahidi kuhudhuria; na waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ubelgiji aliyekuwa amepanga kuhudhuria sherehe hizo …

Dk Shein awataka wakufunzi wa uwalimu kubadilika

Na Rajab Mkasaba, Pemba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka waalimu wa ualimu kubadilika katika utoaji wa mafunzo ya elimu, ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mpya za ufundishaji katika kuwatayarisha walimu. Wito huo ameutoa leo huko Mchanga Mdogo, Mkoa wa Kaskazini Pemba kaika uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa …

Kamati ya Kuzuia Ukatili kwa Wanawake yazinduliwa Tanzania

Na Mwandishi Wetu KAMATI Maalumu itakayofanya kazi ya kuzuia vitendo vya kikatili kwa Wanawake nchini Tanzania imezinduliwa jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ya Kitaifa imezinduliwa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anna Maembe. Akizungumza katika uzinduzi wa kamati hiyo, Maembe alisema licha ya uwepo wa kauli za kupinga vitendo vya unyanyasaji …

Mtanzania aombewa ITC Uingereza

*Mzambia kuichezesha Twiga Stars CHAMA cha Mpira wa Miguu Uingereza (FA) kimetuma maombi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) mchezaji Douglas Didas Masaburi ili ajiunge na klabu ya nchini humo. Masaburi mwenye umri wa miaka 21 anaombewa ITC ili ajiunge na klabu ya Coventry Spartans akiwa mchezaji wa ridhaa. Coventry Spartans iko …