Na Mwandishi Maalumu, Ikulu RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete leo, Desemba 22, 2011, amekatisha mapumziko yake ya sikukuu na kurejea Dar es Salaam kujionea madhara na uharibifu wa mafuriko pamoja na kutoa mkono wa pole kwa waliopoteza ndugu, kuumia ama kuharibiwa mali zao na mafuriko hayo. Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere …
Dk Shein amtumia JK rambirambi ya maafa
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete kufuatia maafa yaliotokana na mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha tokea juzi mjini Dar es Salaam. Katika salamu hizo, Dk. Shein amepokea kwa masikitiko makubwa, taarifa ya mafuriko …
Serikali yatenga ardhi kwa wakazi wa mabondeni
*Vifo vyaongezeka na kufikia watu 20 Na Joachim Mushi IKIWA ni siku moja tangu kuibuka kwa maafa makubwa ya mafuriko baada ya kunyesha mvua kubwa za siku mbili mfululizo jijini Dar es Salaam, iliyoleta athari kubwa kwa wananchi na kusababisha vifo. Serikali imesema imetenga eneo maalumu lenye ukubwa wa hekari 2,000 ambalo litatumika kuwagawia viwanja wakazi wa mabondeni jijini Dar …
Vodacom yatoa pole maafa Dar es Salaam
*Yatoa mil. 30, wateja wake kuchangia kupitia Red Alert na M-Pesa Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepokea kwa masikito taarifa za mafuriko yaliosababisha maafa makubwa Mkoa wa Dar es Salaam yaliyogharimu maisha ya watu kufutia baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini na sehemu nyingine za nchi. Hali hii inatoa uhitaji wa taifa kushikamana na kuwafariji …
Vijana wa Sudan Kusini ‘Watekwa Nyara’
KUMEKUWA na wasiwasi kuwa huenda raia wa Sudan Kusini wanaoishi Mjini Khartoum, Jamhuri ya Sudan wanatekwa nyara na makundi ya wapiganaji, zoezi linalodaiwa kuanza hivi karibuni. Inadaiwa baadhi ya makundi yenye silaha kutoka Sudan Kusini yameweka kambi mjini Khartoum na kuendeleza maasi dhidi ya serikali ya Sudan Kusini, ikiwemo utekaji. Taarifa zaidi kutoka nchini humo zinasema Serikali ya Sudan imeshutumiwa …
JK amteua Jaji Lubuva kuwa M/Kiti wa NEC
*Ateua pia msaidizi na mtendaji wa NEC Na Mwandishi Wetu RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemteua Jaji mstaafu, Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC). Aidha, Rais Kikwete amemteua Jaji mstaafu, Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi. Kwa mujibu …