YAYA TOURE mchezaji bora CAF

Mcheza kiungo wa klabu ya Manchester City na Timu ya Taifa ya Ivory Coast,Yaya Toure amechaguliwa kua mchezaji bora wa soka na Shirikisho la soka ya Afrika(CAF) Mchezaji huyo mashuhuri alipitia mchujo wa ushindani na Seydou Keita kutoka Mali anayechezea klabu ya Barcelona na Andre Ayew wa Ghana pia klabu ya Olympique Marseille. Toure, mwenye umri wa miaka 28, alichaguliwa …

Tshisekedi na ndoto za Urais-DRC

Kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi amejiapisha mwenyewe nyumbani kwake baada ya kuzuiliwa kutoka nyumbani. Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameziba njia ya kwenda kwenye uwanja wa michezo ambapo kiongozi mkuu wa upinzani alipanga kujiapisha. Etienne Tshisekedi amekataa kukubaliana na ushindi rasmi wa Rais Joseph Kabila katika uchaguzi uliofanyika Novemba. Mwandishi wa BBC Thomas Hubert kwenye mji mkuu, Kinshasa …

Simba, Yanga kuchangia wahanga wa mafuriko

KLABU za Yanga na Simba zitacheza mechi za kimataifa za kirafiki na mabingwa wa Malawi, Escom United siku ya Jumatatu na Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuchangia watu waliokumbwa na janga la mafuriko jijini Dar es Salaam. Kwa siku tatu mfululizo sasa mvua kubwa zimekuwa zikinyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha baadhi ya watu kufariki, wengine …

Dk Nchimbi atoa siku 75 kusakwa vazi la taifa

Na Beatrice Mlyansi na Benjamin Sawe WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi ameitaka kamati mpya ya kubuni vazi la taifa kukamilisha mchakato wa kupata vazi hilo ndani siku 75 ili liweze kupelekwa kwenye Baraza la Mawaziri kwa uamuzi zaidi. Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kamati hiyo, Waziri Nchimbi amesema kazi ya …

Yajue mafanikio ya SIDO mkoani Ruvuma, miaka 50 ya Uhuru

Na Mwandishi Wetu Ruvuma SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 28 ya mwaka 1973. Shirika lilianzishwa kwa malengo ya kupanga, kuratibu na kutoa huduma zitakazosaidia kuendeleza ustawi wa viwanda na biashara ndogo nchini. Shirika hilo limekuwa likihusika na kutoa huduma za kuendeleza teknolojia, kutoa mafunzo kwa ujasiriamali na ugani, masoko, habari na fedha. Katika …