Leo ni leo, nani mbabe kati ya Maneno Osward na Rashid Matumla

Mratibu wa pambano la Ngumi za kulipwa, Shabani Adios ‘Mwayamwaya'(katikati), akiwashuudia mabondia, Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ kushoto na Rashidi Matumla ‘Snake Man’, wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito leo, kwa ajili ya pambano lao, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Helnken Mtoni KIjichi, Dar es Salaam siku ya X-Smas. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Shivji amkosoa Kikwete kuhusu katiba

MWENYEKITI wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Profesa Issa Shivji amekosoa Sheria ya Mchakato wa Kuundwa kwa Katiba mpya iliyosainiwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni na kusema kuwa ni mbovu na haitazaa katiba bora. Novemba 29 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 huku kukiwa na malumbano makali kutoka asasi …

Yanga Tabata kukutana Boxing Day

Na Mwandishi Wetu WANACHAMA wa klabu ya Yanga tawi la Tabata wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa mwaka utakaofanyika kesho, Jumatatu (26 Desemba, 2011) kwenye Ukumbi wa Ofisa Mtendaji Kata huku ajenda kubwa ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa tawi hilo, Michael Warioba alisema, wanachama …

Salamu za Krismas na Mwaka Mpya

UONGOZI na wafanyakazi wa Gazeti Tando la dev.kisakuzi.com unapenda kuwatakia heri ya Siku Kuu za Chrismas na Mwaka Mpya 2012 wasomaji, wachangiaji na wote wenye mapenzi mema. Mungu awajalie kila jema na kuwawezesha kusherehekea siku kuu zote kwa amani na utulivu. Upendo na baraka za Mungu pia ziingie kwa mipango ya kila mmoja katika mwaka mpya wa 2012. Kutoka Utawala …

Kafulila bado ni mbunge

  Hatima ya ubunge wa David Kafulila aliyetangazwa kuvuliwa uanachama wa NCCR-Mageuzi na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, hadi sasa bado kitendawili. Hali hiyo imedhihirika baada ya Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza, kueleza wamekwisha kuliarifu Bunge kuhusu uamuzi huo wa NEC dhidi ya Kafulila, huku Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, akisema bado hajaiona taarifa yoyote ya chama …