Waathirika wa mafuriko bado wanahitaji misaada

NDUGU zetu waliopatwa na janga la mafuriko bado wanahitaji misaada yetu Watanzania tafdhal endelea kuchangia kwa Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja anaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS wenye neno MAAFA na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990. Jinsi ya kuchangia …

Wakazi Kota za Bandari Kariakoo wagoma kuvunjiwa

WAKAZI wa Kariakoo Kota za Bandari Kata ya Gerezani wameitaka serikali kutowahamisha wala kuwavunjia nyumba zao hadi hapo kesi yao iliyopo mahakama kuu kitengo cha Ardhi itakapo kamilika. Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa mtaa huo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuwa nyumba hizo walinunua kutoka serikali na kupewa mkataba. Alisema eneo hilo linataka kuchukuliwa …

Kombora mbio za urais 2015

*Mch. Lusekelo asema kuwaza sasa ni utoto wa moyo, *Sitta asema urais unakuja wenyewe MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo amesema mbio za urais za 2015 zitalipeleka taifa kubaya huku akisema wanaofanya harakati hizo kwa kasi hivi sasa ni sawa na watu wenye “utoto wa moyo.”Wakati mchungaji huyo akisema hayo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema …

Maaskofu waonya posho mpya, ufisadi

*Wasema tusipokuwa makini tunauza uhuru wetu MAASKOFU nchini jana walitumia ibaada ya Krismasi, kuzungumzia mambo kadhaa ya kitaifa yakiwamo nyongeza ya posho za wabunge na mchakato wa katiba mpya na kuonya kuwa Watanzania wasipokuwa makini watauza uhuru wao.Wakihubiri kwa nyakati tofauti katika makanisa mbalimbali viongozi hao wa kidini walisema Tanzania ambayo sasa imefikisha miaka 50 ya uhuru wake, inahitaji viongozi …

Mpambano wa Matumla Osward hakuna mbabe

MPAMBANO kati ya mabondia Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ umemalizika jana jijini Dar es Salaam huku mabondia hao wakitoshana nguvu. Katika pambano hilo lililokuwa na ushindani mkubwa lilimalizika huku mabondia wote wakiibuka na pointi 99 kwa 99, hivyo majaji kulazimika kutoa droo kwa wababe hao.