Msuguano kati ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, umefichua siri nzito, baadhi zikihusisha njama za kutaka kufukuzwa kwa mbunge huyo katika chama na nyingine kuhusishwa kwa harakati zake za sasa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa. Siri hizo ambazo ziliwekwa hadharani jana na Hamad, baadhi …
Washukiwa ugaidi waachiliwa Kenya
WATU hao ambao ni raia wa Kenya na picha zao zilisambazwa kwa umma kabla, walijisalimisha wenyewe kwa wakuu Jumamosi iliopita. Vita dhidi ya ugaidi nchini Kenya vimekosolewa, huku polisi wakishutumiwa kutokuwa makini katika uchunguzi wao . Msemaji wa polisi nchini Kenya, Eric Kiraithe aliiambia BBC, kwamba bado wako imara katika kupambana na ugaidi licha ya washukiwa hao kuachiliwa huru. Na …
Msimamo mkali wa dini wapingwa Israil
Rais Shimon Peres wa Israil alisema wachache nchini Israil wanafanya vitendo vya aibu na wanavunja umoja wa taifa. Aliwahimiza watu wajiunge na maandamano hayo katika mji wa Beit Shemesh, karibu na Jerusalem. Mji huo umezusha hasira nchini Israil, tangu msichana wa miaka minane aliposema anaogopa kwenda shule, baada ya wanaume wa Kiyahudi wenye msimamo mkali kumtemea mate, na kumshutumu kuwa …
Mahakama Kuu yasitisha Kafulila kuvuliwa ubunge
MBUNGE wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila amepata amri ya Mahakama Kuu ya kuzuia utekelezaji wa uamuzi wa chama chake kumvua uanachama.Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, ilimvua uanachama Kafulila, Desemba 18, mwaka huu, siku 10 baada ya kumwengua kwenye nafasi ya Katibu Mwenezi wa chama hicho kwa tuhuma za kutoa siri za chama. Amri hiyo ya Mahakama Kuu imetolewa siku chache …
Hali ya Hewa: Mafuriko makubwa yanakuja Dar
*Yasema Alhamisi hadi Jumamosi kuwa siku mbaya zaidi, pia kuyakumba maeneo mengine nchini MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya kuendelea kunyesha mvua kubwa zaidi katika siku 10 zijazo, huku ikizitaja Alhamisi hadi Jumamosi kuwa ni siku za mafuriko mengine makubwa zaidi katika jiji la Dar es Salaam. Wakati TMA ikitoa tahadhari hiyo, Shirika la Reli Tanzania …