WATU takriban 15 wameuwawa na wengine 79 kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea katika mji mkuu wa Myanmar, Yangon. Maafisa wanasema mlipuko huo ulisababisha moto kwenye ghala linalomilikiwa na serikali, ambao ulienea kwa kasi katika makazi ya watu na majengo mengine yaliyokuwa karibu, mengi yao yakiwa ya mbao. Wazima moto wanaendelea na juhudi za kuuzima moto huo na kuzitafuta maiti. Duru za …
Kesi ya Mubarak kuendelea Misri
KESI ya aliyekuwa rais wa zamani wa Misri ,Hosni Mubarak inaanza imeanza tena tarehe 28.12.2011 mjini Cairo, baada ya kipindi cha miezi mitatu kilichoshuhudia machafuko ya umwagaji damu na vyama vya Kiislamu vikishinda uchaguzi wa bunge. Mubarak mwenye umri wa miaka 83 anashtakiwa kwa kuamuru mauaji ya watu takriban 850 wakati wa maandamano ya mapinduzi ambayo hatimaye yalimuondoa madarakani. Anakabiliwa …
Demba Ba achaguliwa kikosi cha Senegal
Senegal imetaja kikosi chake imara cha wachezaji 23 kitakachoiwakilisha nchi hiyo katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, huku kikiongozwa na mpachika mabao hatari katika Ligi Kuu ya Kandanda ya England, Demba Ba. Mfungaji hodari msimu uliopita katika Ligi ya Ufaransa Moussa Sow n mshambuliaji wa klabu ya Freiburg Papiss Demba Cisse pia wamo katika kikosi hicho. Simba hao …
Utovu wa nidhamu wamgharimu Suarez
Taarifa za hivi punde za michezo zinasema mshambuliaji wa klabu ya kandanda ya Liverpool, Luis Suarez amesimamishwa kucheza mechi moja na kutozwa faini ya paundi 20,000 na ameonywa kuchunga tabia yake siku zijazo baada ya kukiri mashtaka yaliyoainishwa na Chama cha Soka cha England juu ya utovu wake wa nidhamu. Suarez hatacheza mechi ya siku ya Ijumaa Liverpool watakapopambana na …
Korea Kaskazini yamzika Kim Jong -il
Korea Kaskazini inafanya maziko ya kitaifa ya kiongozi wake Kim Jong-il huku msafara mkubwa wa magari yaliyosindikiza jeneza la kiongozi huyo ukipitia mji mkuu Pyongyang. Picha cha runinga zimeonyesha maelfu ya wanajeshi wakitoa heshima za mwisho kwa picha ya kiongozi huyo iliyopitia kwenye barabara za mji. Mridhi wa uwongozi ambaye ni mwanawe wa kiume Kim Jong-Un amezindikisha jeneza la babake …