RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Desemba 30, 2011, alifanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Mkuu na pia amefanya uhamisho wa Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, inasema kuwa, Fanuel Mbonde, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu, anahamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria, na Alphayo Kidata, Naibu …
JWTZ yawasaidia chakula waathirika wa mafuriko Dar
Na Mwandishi Wetu JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ) limetoa msaada wa vyakula vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 25, kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40. Akikabidhi msaada huo jijini Dar es Salaam Brigedia Jenerali Cylil Ivor Mhaiki kwa Niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali …
JK atuma rambirambi kifo cha Halima Mchuka
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana, kuomboleza kifo cha mtangazaji maarufu wa shirika hilo, Bi Halima Mohammed Mchuka ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Desemba 29, 2011 kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam. “Nimepokea kwa huzuni habari za kifo cha …
Vodacom yachangisha mil 6,284,000 kwa waathirika wa mafuriko Dar
*Yawataka wananchi kuendelea kuchanga KAMPUNI ya Vodacom Tanzania inawashukuru wote ambao tayari wameshaonyesha upendo wao kupitia kampeni ya “Red Alert” na kufanikisha kukusanya shilingi 6,284,000/= kati ya December 22, 2011 hadi December 27, 2011. Tunapenda kutoa wito wa kuendelea kuchangia Ndugu zetu waliopatwa na janga la mafuriko kwani bado wanahitaji misaada yetu, kwa Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja …
TFF yamlilia mchezaji Rashid Moyo
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa, Rashid Moyo kilichotokea usiku wa Desemba 25 mwaka huu kwao Msambweni, Tanga. TFF imesema hayo leo katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura. Katika taarifa hiyo Wambura amesema Moyo …
Bondia Super ‘D’ ajivunia mafanikio 2011
Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA bondia wa ngumi za kulipwa, Rajabu Mhamila ‘Super D’ na kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti ya Mkoa wa Ilala kimichezo amesema anajivunia mafanikio aliyoyapata katika mchezo wa ngumi kipindi cha mwaka 2011. Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam Super ‘D’ alisema moja ya mafanikio hayo ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi na …