Waumini Kanisa la Kikristo kujengewa uwezo

Na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es Salaam WASHIRIKI zaidi ya 200 wa Kanisa la Kristo kutoka sehemu mbalimbali nchini wanatarajia kukutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujengewa uwezo kuanzia Jumatatu hadi Jumatano. Hatua hiyo inalenga kuwajengea uwezo kwa ajili kuwafanya waondokane na utegemezi. Kauli hiyo itolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Kanisa la Kristo Magomeni …

Iran yajaribu kombora jipya

IRAN inasema imefanya jaribio la kurusha kombora la masafa ya wastani. Jaribio hilo lilifanywa wakati wa mazoezi ya jeshi karibu na Hormuz, mlango unaounganisha Ghuba na Bahari ya Hindi. Jeshi la wanamaji la Iran linasema siku ya mwisho ya mazoezi Jumatatu, meli zitaweza kupita kwenye njia ya Hormuz, ikiwa tu jeshi hilo litaziruhusu. Mkondo wa Hormuz ni njia inayopitwa na …

Dk. Shein ahaidi neema 2012 kwa Wazanzibar

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) mwaka 2012 imeahidi kuimarisha miundombinu na ubora wa huduma za jamii zikiwemo elimu, afya na maji safi na salama ili kwa pamoja visaidie kufikia lengo la kukuza uchumi na kupunguza umasikini, bila ya kuisahau dhamira kuu ya Mapinduzi ya Kilimo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. …

Shambulio la Garissa Al-shabaab wausishwa watano wauwawa

WATU WATANO wameuwawa na zaidi ya 20 kujeruhiwa kwenye klabu ya starehe mjini Garissa, kaskazini-mashariki mwa Kenya. Washambuliaji walirusha maguruneti kwenye klabu hiyo na kisha kuwapiga risasi watu waliojaribu kukimbia. Mji wa Garissa uko karibu na mpaka wa Somalia ambako jeshi la Kenya lilingia mwezi wa Oktoba, kuwaandama wapiganaji wa al-Shabaab. Polisi wanasema watu waliohusika na al-Shabaab huenda walifanya shambulio …

Katibu Mkuu Kiongozi aapishwa na Rais Kikwete Ikulu

RAIS wa Tanzania akimuapisha Katibu Mkuu Kiongozi Mpya, Balozi Ombeni Sefue kushikilia nafasi hiyo. Kuapishwa kwa Balozi Sefue ni kunakamilisha kazi ya Rais Jakaya Kikwete alioifanya juzi baada ya kumteua kiongozi huyo mkuu Ikulu. Balozi Sefue anashika nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo anayemaliza muda wake Desemba 31, 2011. Wasifu wa Balozi Sefue ni mwanataaluma ya diplomasia ambaye tokea …