Kiungo wa Chelsea Michael Essien atarejea uwanjani katikati ya mwezi wa Januari baada ya kupona maumivu ya goti yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Michael Essien kurejea uwanjani mwezi wa Januari Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana hajacheza kandanda msimu huu wote baada ya kuumia kabla ya mechi ya kwanza ya kufungua msimu. Kocha wa Chelsea Andre Villas-Boas amesema Essien anakaribia …
Mwanamuziki Senegal atangaza kugombea urais
MWANAMUZIKI mashuhuri nchini Senegal na mwanaharakati wa kisiasa,Youssou N’dour, ametangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi Februari nchini humo. Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, ambaye anapania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu. Youssou N’dour amehusika na maswala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia …
Al- Mahmoundi kurudishwa Libya
RAIS wa Tunisia, Moncef Marzouki, amesema nchi hiyo haitamuwasilisha kwa mashtaka nchini Libya aliyekuwa waziri mkuu wa Libya, Baghdadi Al-Mahmoudi, bila ya hakikisho kwamba atashtakiwa kwa njia iliyo huru na haki na kwamba atalindwa. Libya inamsaka Bwana Al-Mahmoudi kwa tuhuma za kutumia vibaya mamlaka. Al-Mahmudi alitorokea nchini Tunisia punde baada ya Kanali Gaddafi kupinduliwa na anameshikiliwa nchini humo. Akiwa ziarani …
JK atoa salamu za Mwaka Mpya 2012 kwa Watanzania
Ndugu Wananchi; LEO tunauaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012. Naungana nanyi Watanzania wenzangu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na bahati ya kuiona siku ya leo. Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao hawakujaaliwa kuwa nasi kwa kuwa wametutangulia mbele ya haki. Tuzidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema na sisi tuendelee kumuomba Mola wetu atujaalie rehema …