Fidia ya Kimbangulile kwa Samata yakwama

*TFF yaonya usajili dirisha dogo 2011/2012 KAMATI ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya uenyekiti wa Alex Mgongolwa ilikutana Desemba 30 mwaka jana kupitia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa mbele yake ikiwemo taarifa ya uamuzi wa timu ya Kimbangulile kukata rufani Kamati ya Rufani kupinga uamuzi wake juu ya mchezaji Mbwana Samata. …

TAWIRI yaagizwa kutafiti kutoweka kwa Palahala

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameiagiza taasisi ya utafiti wa wanyamapori (Tanzania Wildlife Research Institute – TAWIRI-) kutafiti sababu za kutoweka kwa mnyama aina ya Palahala (Roosevelt Sable Antelope) katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani mkoani pwani na maeneo mengine walikokuwa wakionekana kwa wingi hapo awali. Rais Kikwete ametoa agizo hilo mwanzoni mwa …

Rais Kikwete apeleka rambirambi CCM

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama kuomboleza kifo cha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Marehemu Athumani Mhina kilichotokea nyumbani kwake Januari Mosi, 2012 kutokana na ugonjwa wa moyo. ”Nimeshtushwa, nimesikitishwa …

Wabunge Dar wawakumbuka Wananchi wao!

*Wampinga Dk Magufuli kupandisha nauli vivuko WABUNGE wa Mkoa wa Dar es Salaam wamepinga hatua ya Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi kupandisha gharama ya kivuko cha Kigamboni kwa asilimia 100 kwa wananchi na kudai hatua hiyo itawaathiri wapiga kura wao kiuchumi hasa wakazi wa Kigamboni. Akizungumza na vyombo vya habari jana Dar es salaam, Katibu wa wabunge hao ambaye ni …

Maisha 2012 hayashikiki-Watabiri

IMETABIRIWA kuwa mwaka 2012 utakuwa mwaka mwengine mbaya kiuchumi kwa bara la Ulaya, ingawa ahuweni ya kiuchumi katika masoko yanayoinukia na Marekani huenda ikaufanya uchumi wa dunia kutokupoteza muelekeo moja kwa moja. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la Reuters, hakuna sababu za kuufurahikia mwaka wa 2012. Mataifa mengi makubwa duniani yanaelekea kwenye mtikisiko wa kiuchumi, masoko …