Rwanda yashambuliwa

TAKRIBAN watu 18 wamejeruhiwa vibaya kufuatia shambulio la gurunedi lililofanyika mjini Kigali. Maofisa wa polisi wamesema hakuna mtu aliyeuawa katika shambulio hilo lilofanyika usiku wa Jumanne. Taarifa zinasema bado haijafahamika waliohusika na shambulio hilo, na tayari upelelezi umeanza. Mwanamke mmoja aliiambia BBC kuwa; “Nilikuwa nakwenda kuchukua simu yangu nikasikia mlipuko mkubwa, tukaanguka hapa na pale, wengi walinilalia wale waliokuwa nyuma …

Kikwete ateua balozi wa Italia na UN

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewateua mabalozi wawili kuiwakilisha Tanzania nchini Italia pamoja na Naibu Balozi wa kudumu Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York. Taarifa hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam, licha ya uteuzi kufanyika tangu Oktoba 12, mwaka jana, 2011. Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Yohana …

HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN KATIKA SHEREHE YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI SEKONDARI YA UZINI KWA NIABA YA SEKONDARI SABA ZINAZOJENGWA KWA UFADHILI WA BENKI YA DUNIA, JANUARI 3, 2012

Assalam Alaykum Naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu (SW) kwa kutujaalia uzima na afya tukaweza kukutana asubuhi ya leo katika hafla hii muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu hususan katika sekta ya elimu. Aidha, nachukua fursa hii kuushukuru uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa mara nyengine tena kunialika katika hafla ya uwekaji wa mawe ya msingi ya …

Jambazi laua askari kwa risasi Arusha

*Lamjeruhi pia Mkuu wa Upelelezi Na Mwandishi Wetu, Arusha KONSTEBO wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha namba F 2218, wa Idara ya Upelelezi, Kijanda Mwandu amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na jambazi. Wakati jambazi hilo likimuua askari huyo pia limemjeruhi kwa risasi Mraribu Msaidizi wa Polisi, ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arusha, Faustine Mafwele . Akizungumza jana …

TFF wamtosa Basena, yamtaka kumalizana na Simba

Na Mwandishi Wetu MALALAMIKO ya Kocha Moses Basena kwa TFF baada ya klabu yake ya Simba kusimamisha mkataba wake yaliwasilishwa mbele ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana Dar es Salaam, kupitia kwa Ofisa Habari wake Boniface Wambura, baada ya kupitia malalamiko hayo, uamuzi wa kamati …