Na Magreth Kinabo-MAELEZO MWENYEKITI mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema atafanya kazi katika taasisi hiyo nyeti ya umma kwa kuzingatia sheria za nchi na Katiba. Jaji Lubuva ametoa kauli hiyo leo mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete katika halfa fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. “Nitaendeleza shughuli za tume …
Kanisa lashambuliwa Nigeria
MAOFISA wa Polisi nchini Nigeria wamesema kuwa watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wamewauwa watu watatu katika shambulio walilolifanya kwenye kanisa moja, Mji wa Gombe ulioko Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Mchungaji wa kanisa hilo, John Jauro amesema waumini wake walishambuliwa wakiwa wakisali sala za jioni. Mchungaji huyo wa Kanisa la Deeper Life ameongeza kuwa mke wake ni miongoni mwa watu waliouawa. …
Ziara ya Kafulila Kigoma yaitesa NCCR-Mageuzi
Joto la kisiasa katika Jimbo la Kigoma Kusini, linazidi kupanda, baada ya baadhi ya viongozi wa Chama cha NCCR-Mageuzi kutoka makao makuu kuingia jimboni humo wakieleza hatua zilizochukuliwa na chama hicho dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, David Kafulila . Viongozi hao ambao wamepata wakati mgumu wakati wakifuatilia ziara ya Kafulila kwa zaidi ya wiki moja tangu alipoanza ziara ya …
Hamad Rashid mwisho
Baraza Kuu cha Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) limewafukuza rasmi viongozi wanne wa chama hicho, akiwemo muasisi wake na Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid Mohammed. Viongozi hao wamefukuzwa baada ya kupatikana na hatia ya kula njama za kukivuruga chama hicho na kutoa tuhuma za uongo dhidi ya viongozi wa kitaifa kwa kuwahusisha na tuhuma za ubadhirifu wa …
Magufuli awavimbia wabunge wa Dar
Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli amesema hayupo tayari kushusha nauli ya kivuko cha Kigamboni kama wanavyoshinikiza baadhi ya wananchi na wanasiasa tofauti na agizo lake la awali. Magufuli ametoa ufafanuzi huo jana alipokuwa akizungumza na wanahabari na kusisitiza kuwa serikali haiwezi kushusha nauli hiyo kwa kuwa viwango vipya vimepitishwa kialali kwa mujibu wa sheria. Amesema …