PrecisionAir kuisafirisha Twiga Stars
Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya ndege ya PrecisionAir imetoa msaada wa tiketi zenye thamani ya sh. milioni 27.8 kwa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) zitakazoisafirisha timu hiyo kwenda na kurudi nchini Afrika Kusini. Twiga Stars Januari 14 mwaka huu inatarajia kucheza na Namibia jijini Windhoek kuwania nafasi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC). Akitangaza msaada huo …
Hamad Rashid asema bado ni mbunge na mwanaCUF
Na Mwandishi Wetu IKIWA ni siku moja tangu Chama cha Wananchi (CUF) kumfukuza uwanachama Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid pamoja na wenzake watatu, mbunge huyo amejitokeza na kusema bado ni mwanachama halali wa CUF. Rashid ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam na kusisitiza yeye bado ni mwanachama kutokana na amri iliyotolewa …
Fukuza fukuza wabunge ‘yamgusa’ Tendwa
*Afikiria kuangalia upya sheria Na Magreth Kinabo–Maelezo, Dar es Salaam MSAJILI wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amesema kwamba ofisi yake inafikiria kubadilisha mifumo ya uchaguzi ili kuweka utaratibu wa kulinda haki za msingi za mpiga kura pale inapotokea chama fulani kinamfukuza uanachama mbunge. Tendwa ametoa kauli hiyo jana Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu mara …