*Ujenzi kuanza, Dk Magufuli ashinikiza likamilike mapema
Hakuna Mzanzibar ambaye hajanufaika na Mapinduzi-Dk Shein
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema hakuna mwananchi hata mmoja wa Zanzibar anaweza kusimama na kupinga kuwa hajafaidika na matunda ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964. Dk. Shein aliyasema hayo kwa nyakati tofauti katika uzinduzi wa barabara sita Kisiwani Pemba zikiwemo barabara ya Chanjani-Pujini, Chanjamjawiri-Tundauwa na Mtambile-Kangani, …
Rais wa Guinea Bissau afariki dunia
RAIS wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha, amefariki dunia katika hospitali moja mjini Paris, nchini Ufaransa, alipokuwa akipokea matibabu. Ofisa mmoja wa Serikali ya Ufaransa leo ametangaza kifo cha kiongozi huyo wa taifa hilo la magharibi mwa Afrika ambalo limekumbwa na misukosuko. Sanha ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 64, alilazawa katika hospitali ya kijeshi ya Val de Grace …
Ni mgomo wa kutisha nchini Nigeria
MGOMO wa nchi nzima umeitishwa nchini Nigeria kupinga kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta ambayo imesababisha shughuli za nchi hiyo kusimama. Maduka mengi, ofisi, shule na vituo vya mafuta nchini humo vimefungwa katika siku ya kwanza na mgomo ulioitishwa na vyama vya wafanyakazi. Taarifa zaidi zinaeleza maelfu ya watu wamekusanyika mjini Lagos na miji mingine kupinga kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta …
16 wajitokeza kuomba ajira ya Ofisa Ligi Kuu
*Kanyenye arejeshewa ulaji FIFA MCHAKATO wa kumpata Ofisa wa Ligi bado unaendelea. Kamati ya Ligi ilipitia maombi ya watu 16 yaliyowasilishwa TFF kwa nafasi ya Ofisa huyo kwa ajili ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza. Mwisho wa kutuma maombi ilikuwa Desemba 28 mwaka jana. Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema maombi yote 16 yalipitiwa ambapo waliopita katika …