Maisha yetu sasa ni chini ya miti na si mabondeni

TAKRIBANI familia 125 za wapangaji ambao walikuwa wanaishi kwenye hifadhi ya muda ya Shule ya Sekodari Benjamin Dar es Salaam sasa wanaishi chini ya miti nje ya lango la kuingilia shule hiyo, eneo la barabara ya Uhuru. Hali hii imekuja baada ya Serikali kuwaondoa katika kambi hiyo pale shule zilipofunguliwa na kusema haina namna ya kuwasaidia wapangaji hao hivyo watafute …

Maseneta wa US wakataa mashoga jeshini

MASENETA wa chama cha Republican nchini Marekani wamepinga pendekezo la kuwaruhusu wapenzi wa jinsia moja kuhudumu wazi katika jeshi la Marekani. Wamedai kuwa uwezo wa jeshi utavurugwa na kurudisha nyuma sera zilizopo zinazofahamika kama ‘Usiulize,Usiseme.’ Maseneta wawili wa chama cha Democrat waliungana na wale wa Republican kutupilia mbali mageuzi ambayo yaliungwa mkono na rais Obama. Rais Obama alipigia debe mabadiliko …

Kashfa ya ngono yamtafuna mgombea urais-Marekani

MWANASIASA mashuhuri anayegombea tiketi ya urais ya chama cha Republicans nchini Marekani, amekanusha madai mapya kuwa alijaribu kumlazimisha mwanamke mmoja kufanya mapenzi naye. Herman Cain anaongoza wanaogombea tiketi hiyo ilikukabiliana na Rais Barack Obama kwenye uchaguzi mwakani. Akizungumza kwenye runinga ya ABC, Bw Cain amesema madai hayo ni ya uongo na atayajibu ipasavyo katika mkutano na waandishi wa habari leo …

Romney atwaa ushindi New Hampshire

MITT Romney amepiga hatua ya kupata tiketi ya chama cha Republican baada ya kupata ushindi katika jimbo la New Hampshire. Romney amepiga hatua kupata tiketi ya Republican Kufikia sasa kura bado zinahesabiwa lakini katika asilimia 19 ya vituo vya kura, Romney alikuwa anaongoza wenzake na asimia 35 ya kura zilizopigwa. Dakika 20 baada ya vituo kufungwa Romney alihotubia wafuasi wake …

Ikulu yapinga kuhusika ugawaji vitalu vya uwindaji

Na Mwandishi Maalumu IKULU imetoa taarifa ya kupinga taasisi hiyo nyeti nchini kuhusika na utaratibu wa ugawaji wa vitalu vya uwindaji. Gazeti la kila siku la Mtanzania la Jumanne, Januari 10, 2012 katika ukurasa wake wa kwanza limechapisha habari yenye kichwa cha habari “Ikulu Yazuliwa Jambo”. Habari hiyo inayowakariri wafanyabiashara wasiotajwa majina mjini Dallas, Texas, Marekani, imedai kuwa Ikulu imeagiza …