Polisi wamuua jambazi aliyeua askari Arusha

*Wengine wanne washikiliwa na Polisi Janeth Mushi, Arusha JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limemuua mtuhumiwa anayesadikiwa ni jambazi, Pokea Samson Kaaya maarufu kama ‘Kaunda’ aliyekuwa akitafutwa na jeshi hilo baada ya kumuua askari namba F.2218, Konstebo wa Upelelezi Kijanda Mwandu kwa risasi ya shingo na kumjeruhi Mrakibu Msaidizi wa Polisi, ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arusha, Faustine …

‘Kunyang’anywa ubingwa hatunitishi nafuata maslahi’

Na Mwandishi Wetu BONDIA Karama Nyilawila ameibuka na kudai kitendo cha kunyang’anywa mkanda wake wa ubingwa wa Dunia wa WBF, na waandaaji wa mashindano hayo hakimsumbui kwani yeye anachoaangalia ni maslahi yake. WBF jana ilitangaza kumnyang’anya ubingwa huo kupitia kwa wasimamizi wa pambano hilo hapa nchini Rais wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST), Emmanuel Mlundwa baada ya kutangaza …

Mzee Kipara azikwa Dar, Rais Kikwete amlilia

Na Mwandishi Wetu WAKATI wasanii mbalimbali, ndugu, jamaa na marafiki wa msanii nguli wa maigizo Mzee Fundi Saidi, maarufu kwa jina la kisanii la Mzee Kipara wakijitokeza jana kumzika msanii huyo, Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete amekitumia salamu za rambirambi Kikundi cha Sanaa cha Kaole kuomboleza kifo cha msanii huyo maarufu na mkongwe. Katika salamu zake za Januari 12, 2012, …

Mohamed Raza ateuliwa kugombea Uwakilishi Jimbo la Uzini

Na Sufianimafoto.blogspot.com, Zanzibar KAMATI Kuu ya CCM imemteua mwanachama wake, Mohammed Raza kuwa mgombea wa Uwakilishi jimbo la Uzini. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema kwamba kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kimempitisha Raza baada ya kuridhika na sifa zake. Nape alisema, Kamati Kuu pia imemteua Makamu …

HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Assalaam Alaykum, Ndugu Wananchi; Kwanza kabisa, namshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma, Aliyetakasika, kwa kutujaaliya kufika siku hii ya leo kuadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, tukiwa wenye afya njema, amani, mshikamano, umoja na furaha. Pamoja na kuadhimisha mwaka wa 48 wa Mapinduzi pia tumekamilisha mwaka mmoja tangu kuanza kwa Awamu ya Saba ya …

Marekani yakerwa maiti ‘kukojolewa’ na askari

WAZIRI wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta amesema video inayoonesha askari wa Jeshi la Majini la Marekani wakikojolea maiti za Wafghanistan ni la “kusikitisha sana”. Alisema, wale walioshiriki katika tukio hilo kwa namna moja au nyingine watachukuliwa hatua “kali sana”. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Asia zinasema video hiyo, iliyowekwa kwenye mtandao, imekusudia kuonesha wanajeshi wanne wa majini wakiwa wamesimama …