*Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Ikulu ajitambulisha MKURABITA
Home Shopping Centre yasaidia Magwepande
Na Mwandishi Maalumu KAMPUNI ya Home Shopping Centre (HSC) imeahidi kujenga kituo cha polisi, vyomba 14 vya madarasa ofisi za walimu na chumba cha kulia chakula kwa ajili ya waathirika wa mafuriko watakaohamia Mabwepande nje ya jiji la Dar es Salaam. Mbali na ahadi hiyo HSC imetoa mifuko 2,000 ya saruji, vyombo vya ndani na taa za sola kwa familia …
Hotuba ya Dk Slaa akihutubia wananchi Mbeya
Tafadhali bofya hapa:- http://mbeyayetu.blogspot.com/2012/01/sikiliza-hotuba-ya-dkt-slaa-alipokuwa.html
CHADEMA wapoteza mbunge ajalini leo
MBUNGE wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Rejea Mtema amefariki dunia leo asubuhi kwa ajali mkoani Pwani. Taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba Mbunge Mtema amefariki dunia papo hapo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka, lilipomshinda akilipita gari lingine eneo la Ruvu mkoani Pwani. Mtema ambaye alikuwa akielekea mjini Morogoro kutokea Dar es Salaam …
Rais Kikwete atembelea Magwepande, Nyika aja juu
Na Joachim Mushi RAIS Jakaya Kiwete jana ametembelea ziara katika eneo la Magwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kukagua miundombinu katika eneo hilo ambalo litakuwa makazi ya watu walioathiriwa na mafuriko katika maeneo ya mabondeni. Akiwa eneo la tukio Rais Kikwete alisomewa taarifa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki juu ya …
TFF yawapa ITC Samata, Ochan na Usajili Yanga, Simba wapita CAF
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji Mbwana Samata na Patrick Ochan waliojiunga na timu ya TP Mazembe wakitokea Simba. TFF ilipokea maombi ya uhamisho huo wa kimataifa Januari 10 mwaka huu kutoka Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (FECOFA) kwa niaba ya TP …