Mtandao Vodacom M-Mpesa waboreshwa

*Kasi yaongezeka, wateja wazidi kufurahia huduma KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imefanya maboresho makubwa katika mfumo unaondesha huduma ya Vodacom M-Pesa kwa lengo la kuendana na kasi ya ukuaji na mahitaji ya huduma hiyo katika soko nchini. Maboresho hayo sasa yanawawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kufanya miamala yao kwa ubora na kasi ya hali ya juu. Mkurugenzi Mtendaji wa …

Dk Shein aipongeza kamati ya Mapinduzi Cup 2012

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameipongeza Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi ‘Mapinduzi Cup 2012’ kwa kufanikisha mashindano hayo makubwa kitaifa. Dk. Shein ametoa pongezi hizo leo alipokuwatana na Wajumbe wa kamati hiyo, pamoja na wafadhili wakubwa wa mashindano ya mwaka huu ambayo yalifikia kilele Januari …

Uwazi katika familia utapunguza maambukizi ya Ukimwi – AMREF

Na Sixmund Begashe SHIRIKA la Utafiti wa Dawa Barani Afrika (AMREF), limesema vita dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini Tanzania itafanikiwa endapo wazazi katika familia watakubali kuwa wazi juu ya masuala ya taarifa juu ya ugonjwa huo. Changamoto hiyo imetolewa juzi mjini Dar es Salaam na mmoja wa maofisa wa Shirika la AMREF nchini Tanzania, Cayus Marina alipokuwa …

Marehemu Rejia Mtema kuagwa Januari 17

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rejia Mtema aliyefariki jana kwa ajali ya gari anatarajiwa kuagwa kesho Januari 17 jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kuelekea Ifakara mkoani Morogoro kwa mazishi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, …

TAMWA waishauri Serikali kuhusu mtihani kidato cha pili

Na Mwandishi Wetu AZMA ya Serikali kurejesha mtihani wa Kidato cha Pili itawezesha wasichana na wavulana wengi kupata elimu ya sekondari iwapo tu serikali, walimu, wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla watatekeleza wajibu wao katika kufanikisha lengo hilo jema kwa taifa. Changamoto hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurungezi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini …