Mbunge CCM aitaka halmashauri kusambaza Katiba kwa Wananchi

Na Janeth Mushi, Arusha HALMASHAURI ya Wilaya ya Arusha imeagizwa kuhakikisha inachapisha nakala za kutosha za Katiba ya nchi ya sasa na kuzitawanya kwa wananchi wake ili waweze kusona na kuelewa kabla ya kushiriki kutoa maoni katika katiba mpya. Changamoto hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye katika mikutano yake ya …

Dk. Bilal apokea mchango wa Wachina kwa waathirika wa mafuriko

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal jana alipokea mchango wa sh. milioni 10 ukiwa ni mchango toka kwa Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba 2011. Mfano huo wa hundi ya sh. milioni …

Kesi ya Mbunge Lema kuanza Februari 7

Na Janeth Mushi, Arusha KESI inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA) na wanachama 18 wa chama hicho inatarajiwa kuanza kusikilizwa Februari 7 mwaka huu badaa ya upelelezi wake kukamilika. Mapema leo mbele ya Hakimu Judith Kamala anayesikiliza shauri hilo, Mwendesha mashtaka wa Serikali, Rose Sulley ameiomba mahakama kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza maelezo ya awali ya kesi hiyo. …

Waliokufa ajali ya meli Italia wafikia watano, 17 hawaonekani

MAITI mbili zimeopolewa tena katika meli kubwa ya kifahari ya abiria ya Costa Concordia iliyozama juzi nchini Italia eneo la Kisiwa cha Giglio. Kupatikana kwa maiti hizo kunafanya idadi ya abiria waliokuwa katika meli hiyo kufikia tano. Mlinzi wa jirani na ajali hiyo alisema maiti za wanaume wawili wazee zimeopolewa katika upande uliozama wa meli, huku taarifa zingine zikidai bado …

Mgomo Nigeria washingwa kupatiwa suluisho, mazungumzo yavunjika

MAZUNGUMZO baina ya Serikali ya Nigeria na Vyama vya Wafanyakazi kuhusu fidia ya bei ya mafuta yamevunjika, na sasa kuna uwezekano mkubwa kwa wafanyakazi wa visima vya mafuta nao watajiunga na mgomo ulioendelea kwa juma zima. Taarifa zinasema katika mkutano wa jana usiku Vyama vya Wafanyakazi viliitaka Serikali irejeshe kwa ukamilifu fidia ya bei ya mafuta, ama sivyo wataendelea kugoma …

Arsenal yalala, Newcastle yaibuka

MATUMAINI ya Timu ya Arsenal kusogelea nafasi nne bora za juu za Ligi ya Soka ya Uingereza yamevurugwa na Timu ya Swansea baada ya kuonesha kandanda murua na kuweza kupata pointi tatu muhimu kwa kuilaza Arsenal mabao 3-2 katika mchezo wa kusisimua. Katika mchezo huo Arsenal ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya nne kwa bao la Robin …