*Yakana kupokea tamko la madaktari Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Afya, Lucy Nkya amesema tamko lililotolewa na Chama cha Madaktari Tanzania la kutoa saa 72 kwa Serikali kuwarejesha madaktari walio katika mafunzo ya vitendo hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pamoja na madai ya kuhamishwa vituo vya kazi halijawasilishwa rasmi wizarani. Naibu huyo alifafanua kuwa madaktari hao hawajafukuzwa kufanya mazoezi …
SBC Tanzania waisaidia Twiga Stars vinywaji
Na Mwandishi Wetu TIMU ya Taifa ya wanawake Twiga Stars Januari 17 mwaka huu imekabidhiwa msaada wa maji ya kunywa na soda ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yake ya marudiano dhidi ya Namibia itakayochezwa Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kampuni ya SBC Tanzania inayozalisha Pepsi, Mirinda na 7up ilikabidhi msaada wa vinywaji hivyo …
Rejia Mtema ni nyota inayongaa – Makinda
Na Mwandishi Maalumu SPIKA wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda amesema aliyekuwa Mbunge wa Viti wa Maalum mkoa wa Morogoro (CHADEMA) Bi. Regia Mtema ni nyota inayong’aa kwani ameweza kuwaunganisha Watanzania wote bila kujali tofauti za kiitikadi zilizopo katika jamii. Ametoa kauli hiyo Januari 17, 2012) wakati akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuuaga mwili wa Regia Mtema kwenye viwanja …
Mahakama ya Rufani Tanzania kusikiliza jinai 33
Na Magreth Kinabo – MAELEZO MAHAKAMA ya Rufani Tanzania itasikiliza jumla ya kesi 33 zinazohusu watu mbalimbali. Kesi hizo ambazo ni za madai na makosa ya jinai zitaanzwa kusikilizwa kuanzia Februari 13, mwaka huu hadi Machi 5, mwaka huu mkoani Arusha. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Naibu Msajili wa John Mgetta Mahakama ya Rufani Tanzania ilieleza kuwa kesi …
Mbowe, Dk Slaa waongezewa mashtaka Arusha
Na Janeth Mushi, Arusha UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kufanya kusanyiko na maandamano yasiyo na kibali inayowakabili viongozi wa ngazi ya juu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), imeahirishwa hadi Februari 21, mwaka huu ambapo washtakiwa watasomewa mashtaka mapya. Aidha katika kesi hiyo washitakiwa hao walikwua wanakabiliwa kwa makosa nane ila baada ya hati ya mashitaka kufanyiwa marekebisho …