Walemavu wanasahaulika mapambano ya Ukimwi

Na Mwandishi Wetu VIKWAZO kadhaa vinavyowakabili watu wenye ulemavu hasa kupata elimu na ufahamu wa kutosha juu ya ugonjwa wa Ukimwi, vinairudisha nyuma jamii hiyo. Walemavu hawa wamekuwa wakishindwa kupata huduma za kijamii zikiwemo za ushauri na elimu kuhusu maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi. Vikwazo vingine ni pamoja na kukosekana kwa miundombinu stahili kwa jamii husika pamoja na …

JK atoa pole kwa wafiwa nyumbani kwa Sumari

Rais Jakaya Kikwete Akimpa pole mjane wa Marehemu Jeremia Sumary, Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani aliyefariki jana asubuhi jijini Dar es Salaam. Hapa ni nyumbani kwa marehemu, Mbezi Beach, Dar es salaam jioni hii Rais Jakaya Kikwete akiweka sahihi kitabu cha maombolezo Rais Jakaya Kikwete akizungumza na ndugu wa marehemu pamoja na Spika Anne Makinda …

Dk. Bilal atoa pole ya msiba wa Sumari Dar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia …

‘Maandamano ya kudai haki hayahitaji kibali’

Na Joyce Ngowi MBUNGE wa Arusha mjini Godbless Lema kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema haogopi kesi za kupigania haki za wananchi hata kama zikifunguliwa 100 kwani thamani ya maisha ni heshima, utu na usafi wa matendo. Lema alisema hayo Dar es Salaam jana alipokuwa nje ya vikao vya Kamati za Bunge zinazoendelea jijini hapa baada ya kuulizwa …

Ligi Kuu ya Vodacom kuanza Jumamosi

Na Mwandishi Wetu MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza keshokutwa (Januari 21 mwaka huu) kwa mechi nne. Moro United itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Mtibwa Sugar itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani. Nayo Toto Africans itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa …

Dk. Batlda Burian amuaga Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Batlda Burian, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kumuaga rasmi kwenda kuanza kazi nchini Kenya baada ya uteuzi wake. Picha na Muhidin Sufiani-OMR