Mashambulio ya wanawake wavaa suruali yakithiri Malawi
TAKRIBANI watu 3,000 wamekusanyika Blantyre nchini Malawi kupinga mashambulio dhidi ya wanawake wanaovaa suruali. Baadhi ya wachuuzi wa kike wiki hii walipigwa na kuvuliwa nguo kwenye mitaa ya mji mkuu, Lilongwe, na Blantyre kwa kutovaa mavazi ya asili. Mmoja aliyeandaa maandamano hayo amesema amewasihi wanawake kujitokeza wakiwa wamevaa suruali na fulana nyeupe kuonyesha kukasirishwa kwao. Rais Bingu wa Mutharika alisema …
Milipuko yatikisa mji wa Kano, Nigeria al-shabab yahusishwa
Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa kwenye milipuko iliyotokea katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria. Vituo vya Polisi pamoja na makao makuu ya Polisi eneo hilo ni miongoni mwa sehemu zilizolengwa katika mashambulizi hayo. Milio ya risasi pia imesikika katika sehemu kadhaa. Kundi la kiislamu la Boko Haram limesema ndilo lililotekeleza mashambulizi hayo. Kundi hilo ndilo limekuwa likiendesha ghasia katika siku …
Wazimbabwe kuwachezesha Twiga Stars
MECHI ya marudiano kusaka tiketi ya kucheza fainali za Nane za Kombe Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia itachezeshwa na waamuzi kutoka Zimbabwe. Waamuzi katika mechi hiyo itakayofanyika Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam watakuwa Rusina Majo Kuda (mwamuzi wa kati) wakati waamuzi wasaidizi …
ZH Poppe yatoa tiketi kwa waamuzi
KAMPUNI ya ZH Hope Limited imegharamia tiketi za waamuzi na kamishna atakayesimamia mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia itakayofanyika Januari 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Mbali ya tiketi hizo za ndege, pia kampuni hiyo itagharamia hoteli (malazi na chakula) kwa kamishna na waamuzi hao …