Rais Kikwete aenda Uswisi kuhudhuria WEF

Na Mwandishi Maalumu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameondoka nchini jioni ya Januari 24, 2012, kwenda Davos, Uswisi, kuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Umoja wa Uchumi Duniani wa World Economic Forum (WEF) unaoanza Januari 25. Katika siku nne za mkutano huo, mbali na kuhudhuria mkutano wenyewe ambao hukusanya viongozi wakuu wa siasa, biashara, uchumi na …

JK aishukuru Cuba ushirikiano wa maendeleo

Na Mwandishi Maalumu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete leo, Januari 24, 2012, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masula ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Cuba, Alberto Velazco San Jose. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete na San Jose wamezungumzia masuala …

TFF yataja viingilio mechi ya Twiga Stars na Namibia

KIINGILIO cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia itakayochezwa Jumapili, Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 2,000. Kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu na kijani. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 36,693 kwenye uwanja huo wenye uwezo …

Yanga yatakiwa kumlipa Njoroge sh. mil 17

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kupitia kitengo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber- DRC) limeagiza klabu ya Yanga kumlipa mchezaji John Njoroge sh. 17,159,800 ikiwa ni fidia kwa kuvunja mkataba wake kinyume cha taratibu. Uamuzi huo wa DRC chini ya Jaji Theo van Seggelen ambaye ni raia wa Uholanzi ulifanywa Desemba 7 …