WAKALA wa Mario Balotelli ameonya mshambuliaji huyo anaweza kuachana na kandanda ya England iwapo ataendelea kutotendewa haki katika matukio mbalimbali. Balotelli, anakabiliwa na adhabu ya kutocheza michezo minne baada ya kushtakiwa na Chama cha Kandanda cha England kwa kitendo cha vurugu. Mshambuliaji huyo wa Manchester City alionekana kumkanyaga kichwani Scott Parker kabla ya kufunga bao la ushindi kwa mkwaju wa …
Naibu Jaji Mkuu Kenya asimamishwa kazi
*Yaundwa tume chini ya Jaji Mtanzania kumchunguza RAIS wa Kenya, Mwai Kibaki amemsimamisha kazi Naibu Jaji Mkuu, Nancy Baraza na kuunda jopo la majaji ambalo litachunguza mwenendo wa kazi wa kiongozi huyo kutokana na tuhuma zinazomkabili. Taarifa zimesema Jaji Baraza, anatuhumiwa kumtishia maisha kwa bastola mlinzi wa duka moja kubwa, Bi Rebecca Kerubo wakati wa mkesha wa mwaka mpya. Jopo …
Ikulu yakanusha habari ya Tanzania Daima
*Yabainisha faida ya ziara ya JK Davos Na Mwandishi Maalumu GAZETI la Tanzania Daima la leo, Jumatano, Januari 25, 2012, kwenye ukurasa wake wa kwanza limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Ndege ya JK utata: Iko nje kwa miezi miwili. Serikali yakwama kuilipia.” Miongoni mwa yaliyoandikwa kwenye habari hiyo ni pamoja na “Ukata unaiokabili Serikali umesababisha kukwama kuilipia ndege hiyo …
Karibu Kisiwani Zanzibar…!
Usafiri wa jumuia mjini Zanzibar bado zinatumika gari ‘maarufu’ kama “Chai Maharage” ambazo bodi lake limeandaliwa mahususi kwa ubebaji abiria. Raha ya usafiri huu abiria hukaa kwa kuangaliana tofauti na ilivyo kwa usafiri wa jumuia kwa Jiji la Dar es Salaam na miji ya mikoa mingine mingi ya Tanzania Bara, ambapo hutumika gari maarufu kama ‘daladala’. Angalia picha ya gari …
ZSTC yanunua zaidi ya tani 4,466 za karafuu kwa wakulima Zanzibar
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar WIZARA ya Biashara, Viwanda na Masoko kupitia Shirika la ZSTC imesema tayari imenunua jumla ya tani 4,466.03 za karafuu kwa thamani ya milioni 66,990.5 kutoka kwa wakulima, hadi kufikia Januari 23, 2012 na bado zoezi hilo linaendelea ikiwa ni wastani wa tani 10 hadi 18 kwa siku. Uongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko …