Pinda asema Serikali itaendelea kuboresha sekta ya umma, sheria na fedha
Na Mwandishi Maalumu WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amesema Serikali itaendelea kufanya maboresho kwenye sekta za umma, fedha, sheria za Serikali za Mitaa ili kuondoa urasimu katika mifumo ya kiutawala. Pinda ametoa kauli hiyo leo mchana Januari 26, 2012 akifungua Mkutano wa Tatu wa kila mwaka wa majadiliano ya kisera baina ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kwenye Ukumbi …
Steven Galinoma afariki dunia!
ALIYEKUWA Mbuge wa Jimbo la Kalenga, Steven Galinoma amefariki dunia leo mapema. Taarifa zaidi zinasema kuwa Galinoma amefariki dunia leo asubuhi mjini Iringa ndani ya gari akipelekwa hospitalini kutokea Kalenga ambako alikokuwa anaishi. Marehemu Galinoma katika enzi za uhai wake amewahi kushika nafasi anuai, mbali na kuwa mtumishi wa Serikali. Aliwahi kuwa Katibu Mkuu Idara ya Ulinzi na Jeshi la …
Tamasha la kuvumbua vipaji Dar (Grassroot)
Na Mwandishi Wetu TAMASHA la mafunzo ya kuhamasisha watoto kucheza mpira wa miguu na kuvumbua vipaji (Grassroot) kwa shule maalum zilizochaguliwa katika Mkoa wa Dar es Salaam linaendelea Februari 3 mwaka huu. Siku hiyo tamasha hilo litafanyika katika Shule ya Msingi Mtoni Kijichi wilayani Temeke kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana. Februari 10 mwaka huu tamasha lingine litafanyika …
Simba kuchezeshwa na Warundi Kigali
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Kiyovu Sport ya Rwanda itakayochezwa jijini Kigali. Waamuzi hao ni Thierry Nkurinziza atakayekuwa katikati wakati wasaidizi wake ni Jean-Claude Birumushahu na Jean-Marie Hakizimana. Mwamuzi wa akiba atakuwa Hudu Munyemana kutoka Rwanda. Kamishna wa mechi …