Pinda asikitishwa na Tanzania Daima

Na Mwandishi Maalumu OFISI ya Waziri Mkuu imesikitishwa na habari iliyochapishwa na gazeti la Tanzania Daima toleo namba 2610 la Januari 26, 2012, kwenye ukurasa wake wa kwanza yenye kichwa cha habari: “Dk. Mwakyembe aipasua Serikali” *Pinda amtaka azungumzie hali yake *Aunga mkono posho za Wabunge kupanda *Adai wanaosaka Urais hawana akili nzuri KWENYE habari hiyo iliyopewa uzito wa juu …

Jamii za Kifugaji wasaidiwa ujenzi wa bweni

Na Mwandishi Wetu, Arusha MASHIRIKA mawili yasiyokuwa ya kiserikali (NGO’s) yanayotoa msaada na ushauri wa kisheria kwa jamii za kifugaji na wawindaji na kutetea haki zao, yametoa msaada wa zaidi ya sh. milioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Yaedachini wilayani Mbulu. Mashirika hayo ni PINGO’s Forum na UCRT ya mkoani Arusha, ambapo wametoa mabati …

Pambano la Yanga na Zamalek kuchezeshwa na Waethiopia

Na Mwandishi Wetu WAAMUZI kutoka Ethiopia ndiyo watakaochezesha mechi namba 7 ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Zamalek ya Misri itakayochezwa Februari 18 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Bamlack Tessema kuwa mwamuzi wa kati …

JKT Ruvu, Yanga kucheza saa 12 jioni

Na Mwandishi Wetu MECHI namba 100 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Yanga itachezwa kesho (Januari 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo. Lakini mechi hiyo sasa itaanza saa 12 kamili jioni badala ya saa 10 kamili jioni. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface …