CUF yamjibu Hamad Rashid, wenzake 10 mahakamani

Wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF) wamewasilisha Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam majibu dhidi ya maombi madogo ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake 10 na kuwataka watoe uthibitisho wa madai waliyoyatoa katika maombi hayo. Maombi hayo madogo yamo kwenye kesi ya msingi iliyofunguliwa na Hamad na wenzake hao katika mahakama hiyo. Katika maombi hayo, Hamad …

Msafara wa Dk Bilal wapata ajali Tanga, wawili wafariki dunia

Na Mwandishi Wetu MSAFARA wa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal umepata ajali na kuua askari wawili waliokuwa katika moja ya gari la msafara huo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda wanasema ajali hiyo imetokea eneo la Mombo wilayani Korogwe. Taarifa zinasema msafara wa Dk. Bilal umepata ajali ukitokea Wilaya ya Lushoto kuelekea Korogwe baada ya …

Matokeo ya ubunge DRC yatangazwa

*Kabila ashinda viti vingi bungeni MATOKEO ya uchaguzi ya ubunge katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yametangazwa karibu katika maeneo mengi na Chama tawala cha PPRD kimenyakuwa idadi kubwa ya viti 58, huku muungano wa vyama vinavyoiunga Serikali ikiwa imepata idadi kubwa ya viti vilivyonyakuliwa na muungano wa upinzani unaomuunga mkono, Etienne Tshisekedi. Imeichukua tume huru ya uchaguzi katika Jamhuri …

Sudan kuisaidia Tanzania mafunzo kwa madaktari

*Ni wa fani ya upasuaji moyo Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Sudan imesema iko tayari kuleta madaktari ili wasaidie kutoa mafunzo kwa madaktari wa Tanzania hasa kwenye fani ya upasuaji wa moyo (Open Heart Surgery). Hayo yamesemwa leo Januari 27, 2012 na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dk. Yassir Mohamed Ali wakati alipofika kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda …

David Cameron aifagilia Tanzania, asema ni mfano Afrika

Na Mwandishi Maalumu, Davos-Switzerland WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameron ameipongeza nchi ya Tanzania kwa kuwa mfano bora katika kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta za Kilimo na Elimu barani Afrika. David Cameron ametoa pongezi hizo kwa Rais Jakaya Kikwete wakati wa mazungumzo yao hapa Davos, ambapo wote wawili wanahudhuria mkutano wa Kiuchumi Duniani wa kila mwaka, maarufu kama World Economic …