Dk. Shein ataka wananchi wapewe elimu ya maafa na majanga

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema katika kuzingatia uzuiaji wa matukio ya maafa na majanga kuna kila sababu wananchi kupewa elimu na kuzifahamu sababu zake ili jamii ipate uelewa zaidi. Dk. Shein aliyasema hayo jana katika sherehe za uzinduzi wa Jumuiya ya Kuzuia, Kukinga na Kuondosha Maafa …

Pinda sasa awafuata madaktari kwa mazungumzo

*Anazungumza nao leo Jumapili WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda leo Jumapili, Januari 29, 2012 atakutana na madaktari waliofanya mgomo kwenye Ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 4:00 asubuhi. Madaktari hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wanaomba kuonana na Waziri Mkuu na mara zote Waziri Mkuu amekubali kuonana nao lakini hawakutokea. Pamoja na kukubali huko kwa Waziri Mkuu, tarehe 25 Januari 2012 …

Boko Haram wauwawa Nigeria

JESHI la Nigeria linasema limewapiga risasi na kuwauwa wafuasi 11 wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, kaskazini-mashariki mwa nchi. Msemaji wa jeshi alieleza kwamba wapiganaji hao waliuwawa wakati wa mapambano katika mji wa Maiduguri, ambako kundi hilo lilianzishwa mwongo uliopita. Juma lilopita watu kama 185 waliuwawa katika mji mwengine wa kaskazini, Kano, kwenye mashambulio kadha ya mabomu. Boko …

Bia ya Serengeti katika muonekano tofauti, ladha ile ile

Na Joachim Mushi BIA maarufu ya Serengeti inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti nchini (SBL) jana usiku imezinduliwa katika muonekano mpya huku ikibaki na ladha na ubora ule ule wa awali. Hafla ya uzinduzi wa muonekano huo mpya wa bia ya Serengeti umezinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bi. Joyce Mapunjo katika hoteli ya Golden …