Wasafirishaji mizigo EAC wahofia gharama na urasimu

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Samuel Sitta
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Samuel Sitta

Na James Gashumba, EANA

KUMEKUWEPO na maendeleo makubwa katika kupunguza vikwazo vya kibiashara lakini gharama kubwa za usafirishaji zinaibuka kama kikwazo kipya katika kufanya biashara Afrika Mashariki.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Wasafirishaji Mzigo nchini Kenya (KSC), Gibert Langat alitoa maoni hayo jijini Nairobi, wakati wa mkutano wa utendaji wa logistiki wa baraza hilo mwishoni mwa wiki.

“Hali kama hii inategemewa kupunguza ukuaji wa uchumi kwa asilimia moja kwa mwaka, hasa katika nchi za Burundi, Rwanda na Uganda, ambazo maendeleo yao hutegemea usuluhishi wa usafirishaji wa nchi jirani za Kenya na Tanzania,” Langat alisema.

Alisema kuwa gharama za usafirishaji Afrika Mashariki zilikuwa kati ya asilimia 60-70 juu ukilinganisha na Marekani na Ulaya. Zilikuwa pia asilimia 30 juu kulinganisha na Sudan ya Kusini, taifa jipya barani Afrika. Hali hii katika Afrika Mashariki inatoa wingu zito katika ukuaji uchumi, aliongeza.

“Bandari za Dar es Salaam na Mombassa kwa pamoja zimekuwa zikikabiliwa na ongezeko la kila mwaka la mizigo la asilimia 8.8 linalotokana na kukua kwa biashara kikanda. Bandari hizi kwa muda sasa zimekuwa pia zikikabiliwa na tatizo la ucheleweshwaji upakuzi wa mizigo na msongamano,” alisema.

Hata hivyo, marekebisho kadhaa yanatarajiwa kufanyika, ikiwemo wiki ya operesheni ya masaa 24 na siku saba, ujenzi wa viambajengo vya nyongeza na utumiaji wa mitambo inayojiendesha yenyewe katika zoezi la upakuaji wa makontena. Pia kutakuwepo na uboreshaji wa kumbukumbu na utoaji na ukaguzi wa mizigo.

Ukanda wa Kaskazini, unaojumuisha Mombasa kuelekea Uganda, Rwanda na Burundi, Kaskazini mwa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Sudan ya Kusini, Ethiopia na Somalia hutoa kiwango cha mizigo yenye ujazo zaidi ya tani millioni 10 na ujumla wa usafirishaji na ubadilishaji meli kwa zaidi ya tani millioni mbili.

Wakati Ukanda wa kati unaounganisha Dar es Salaam hadi Burundi, Rwanda, Uganda, Malawi, Zambia na DR Congo pia unatoa kiwango cha mizigo sawa na ukanda wa Kaskazini.

“Biashara katika kanda hizi ina mgongano chanya katika eneo hili na juhudhi nyingi zimefanyika kuongeza ufanisi wake, “ alisema. Hata hivyo, alibainisha kuwa ufanisi umekuwa ukipambana na gharama za juu za usafirishaji, upungufu wa miundo mbinu halisia na sera za kitaifa ambazo haziendani na malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mtangamano wake.

Ili kuondoa changamoto katika usafirishaji na lojistiki katika eneo hilo, Langat alishauri wafanyabiashara na watunga sera kwa pamoja kuwa na uelewa wa vikwazo vilivyopo.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.