Rehmtullah kufanya onesho kabambe la mitindo

Rehmtullah kufanya onesho kabambe la mitindo
Rehmtullah kufanya onesho kabambe la mitindo

Na Mwandishi Wetu

MWANAMITINDO maarufu nchini, Ally Rehmtullah ameandaa onesho kubwa la kipekee la mitindo nchini litakalofanyika Septemba 8, 2012 katika jiji la Dar es Salaam na kuonyeshwa moja kwa moja katika mtandao wa www.ar.co.tz ambapo pia atazindua rasmi kazi zake mpya za mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanaume na wanawake.

Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Rehmtullah amesema dhumuni la kuandaa onesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha aina mpya ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati zake za kuinua kiwango cha kazi za mitindo ndani ya nchi.

Mesema amepanga kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini ili kazi za wanamtindo na wabunifu wa mavazi ziweze kupenya kwenye soko la ndani na la Afrika mashariki na kati wakati tayari kuna soko la pamoja katika jumuiya ya Afrika mashariki.

Rehmtullah amesema kwamba onesho hilo litakuwa la kipekee kwa sababu mavazi na onesho litapambwa na rangi nyeupe, ubunifu wa hali ya juu pamoja na muonekano mpya wa mavazi yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza kuendana na utamaduni wa mwafrika.

Amesema onesho hilo litakalofanyika katika hoteli ya Serena litapambwa na wasanii mbalimbali wa muziki na wacheza shoo kutoka sehemu mbalimbali.

Rehmtullah amesema onesho hilo itakuwa ni nafasi ya kipekee kwa yeye binafsi kuonesha muonekano mpya wa tasnia ya mitindo hapa nchini na nje ya nchi ili kuonyesha ni kwa jinsi gani wanamitindo wa kitanzania wanavyoweza kuonyesha kazi zao.

Ameongeza kuwa tasnia ya mitindo kwa ujumla ina nafasi ya kipekee kwa wanamtindo chipukizi kujitokeza na kuonesha kazi zao kwa watu mbalimbali hasa washika dau katika sekta hiyo.

Onesho hilo linategemewa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 400 wakiwemo viongozi mbalimbali kama mawaziri, wabunge, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mashirika mbalimbali. Onesho hilo litakuwa ni la mialiko maalum na limepewa jina la Ally Rehmtullah 2013 collection.

Wadhamini wa onesho hilo ni Mercedez Benz, Belvedere Vodka, DULUX, RAHA, HUGO DOMINGO, THE Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm Plant, Creative Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia Properties, Dar es Salaam Serena Hotel, Quality Furniture na Mx Carter, pamoja na Blog za Missie Popular na MO Blog.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.