Papa FrancisMAELFU ya waumini wa Kanisa Katoliki wanahudhuria misa mjini Havana ambayo itaongozwa na kiongozi wa kanisa hilo, Papa Francis ambaye anafanya ziara nchini humo kwa mara ya kwanza. Katika ujumbe wake, Papa Francis amezitaka Marekani na Cuba kuendelea kuboresha uhusiano kati yao. Akizungumza kwenye uwanja wa ndege wa Havana anapoanza ziara nchini Cuba na Marekani, papa Francis alipongeza uhusiano ambao umeshuhudiwa kati ya nchi hizo. Rais wa Cuba Raul Castro amemshukuru papa Francis kwa jitihada zake kurejesha uhusiano kati ya Cuba na Marekani. Akijibu hayo Rais wa Cuba Raul Castro amemshukuru papa kwa wajibu wake katika kusaidia kurejesha uhusiano kati ya Cuba na Marekani.
Hii ndiyo ziara ya kwanza anayofanya papa Francis nchini Cuba baada ya kulakiwa na umati uliokuwa ukipeperusha bendera za Cuba wakati msafara wake ulikuwa ukipita katika mitaa ya mji wa Havana. -BBC