JK Amteua Rished Bade kuwa Naibu Kamishna wa Mapato

Rished-Bade

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished Bade kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Taarifa iliyotolewa Jumatano, Septemba 19, 2012 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo umeanza Jumatatu wiki hii, Septemba 17, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Bade alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Mortgage Finance Co. Ltd.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.