




WAZIRI wa Fedha Saada Mkuya Salum amefanya ukaguzi wa ghafla katika baadhi ya maduka Mkoani Dodoma ili kuona kama maelekezo ya Serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFD yanatekelezwa ipasavyo. Katika ukaguzi huo ambao ulihusisha maduka ya kuuza thamani za majumbani,nguo na maduka ya kuuza bidhaa mchanganyiko (Min supermarket), Waziri akiongozana na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliagiza kufungwa kwa maduka yote ambayo yamekaidi agizo la Serikali la matumizi ya mashine EFD mpaka pale watakaponunua na kuzitumia ipasavyo mashine hizo.
Aidha Mh.Waziri amewataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuisaidia Serikali kuwafichua wafanyabiashara wasio waaminifu na ambao wanapelekea kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetumika katika kuboresha huduma za kijamii.
