Hizi Hapa Sera za Fredrick Mwakalebela Mgombea Urais TFF

  MGOMBEA Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela ametaja mambo kumi atakayo fanya katika kuinua mpira hapa nchini kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF. Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa kampeni yake Mwakalebela amesema kuwa kwa kuanza ataanza na Utawala bora kwa Kuweka misingi ya wazi katika mapato na matumizi ya TFF, …

Viongozi Waanzilishi TAPSEA Walalamikia Uchaguzi wa Chama Chao

MGOGORO wa uongozi ndani ya Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) umeingia katika hatua tata baada ya viongozi waanzilishi wa chama hicho kulalamikia uchaguzi uliopangwa kufanyika Mai 30, 2015 mjini Dodoma ilhali kuna mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho ukiendelea. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya viongozi wenzake Mwenyekiti wa TAPSEA, Pili Mpenda ambaye pia ni …

David Cameron Ashinda Uchaguzi, Mpinzani Wake Ajiuzulu

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameron amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo jana. Chama chake cha Conservative kimepata viti 330 huku kile cha leba kikijipatia 232. Cameron alisema anapania kuendelea kuiongoza Uingereza kwa umoja. Shirika La BBC lilikisia kuwa Cameron na Chama chake angepata ushindi wa maeneo bunge 329. Chama cha Leba kimepata pigo kubwa huko Scotland …

Boko Haramu Wasababisha Uchaguzi Kuahirishwa

MKUU wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria, Attahiru Jega, amesema upigaji kura hauwezi kufanyika nchini humo Jumamosi ijayo kwa sababu wanajeshi wanaotakiwa kulinda vituo vya kupigia kura wanatumika kupambana na kundi la Boko Haram. “Hatari ya kutumia vijana wetu katika jeshi na kuwataka watu watumie haki yao ya kidemokrasi, katika hali ambapo hawawezi kuhakikishiwa usalama wao, ndio jukumu letu kubwa. …