Na Janeth Mushi, Arusha KESI ya kupinga matokeo ya Ubunge dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), inatarajiwa kuanza kusikilizwa Jumatatu mbele ya Jaji Aloyce Mujulizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha. Habari za ndani kutoka mahakamani hapo zinasema kuwa waliofungua kesi hiyo ni Musa Hamisi Mkanga na wenzake dhidi ya Lema na Mwanasheria wa Serikali, katika kesi …
Gwaride la ‘FFU’ kuendelea Markt, Steinhude!
FFU wa Ngoma Africa Band wanatarajia kutingisha Jukwaa la Afrika Markt, Steinhude, Ujerumani. Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya (Ngoma Africa Band) aka FFU, wamepanga kutumbuiza katika onesho jingine kubwa la wazi mjini Steinhude am Meer, jirani na Hannover, nchini Ujerumani Jumamosi ya Septemba 3, 2011 saa 12.00 jioni. Mapromota wa muziki huko ughaibuni wamehamua kuifanyia kweli …
Polisi Zanzibar yawataka wauza vileo kujilinda wenyewe
Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi- Zanzibar JESHI la Polisi Zanzibar limewaagiza wamiliki na wafanyabiashara wa baa visiwani humo kuchukua tahadhari kwa kuweka walinzi imara katika maeneo yanayozunguuka nyumba za biashara hiyo ili kuepuka matishio ya uchomwaji wa baa zao. Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kua tahadhari hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa …
Maaskofu: Hotuba ya Rais Kikwete nzito
Thursday, 01 September 2011 21:12 MAKANISA nchini yamesema hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyotoa juzi katika Baraza la Idd ni nzito na kwamba, kama angekuwa anatoa hotuba kama hizo, matatizo mengi ya nchi yangekuwa yamepata ufumbuzi.Katika baraza hilo pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete akijibu risala ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, (Bakwata) alizungumzia mambo muhimu kuhusu taifa ikiwa ni …
Rais Kikwete awatembelea majeruhi Basi la Champion
Rais Dk. Jakaya Kikwete akimfariji, Winston Chinduge mkazi wa Gairo, mkoani Morogoro ambaye ni mmoja wa majeruhi wa Basi la Champion lililopata ajali juzi mkoani Dodoma. Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. (Picha na Ikulu)
Wabunge Zimbabwe wagoma kutahiriwa
WABUNGE wanaume nchini Zimbabwe wameonekana kutokukubaliana na wito wa kutaka kutahiriwa ili kuonesha mfano katika kupambana dhidi ya Ukimwi, BBC imegundua. Naibu Waziri Mkuu, Thokozani Khupe alitoa wito huo, kufuatia ushahidi kuwa wanaume waliotahiriwa wana uwezekano wa kuathirika na virusi vya HIV kwa chini ya asilimia 60. Miongoni mwa wabunge wanane waliozungumza na BBC, mmoja tu alisema atatilia maanani pendekezo …