Prof. Tibaijuka acharuka, afuta viwanja 87 vilivyovamiwa

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeanza kufanya oparesheni maalumu kuhakikisha inayarejesha maeneo yote ya wazi yaliyovamiwa kinyemela maeneo ya Jiji, Miji na katika manispaa. Zoezi hilo linafanywa kwa kusimamiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazia, Prof. Anna Tibaijuka, ameanza katika majiji, miji na Manispaa, na tayari Wizara imefuta hati za viwanja …

Nimekuja Igunga kuchukua ushindi – Mkapa

Na Bashir Nkoromo, Igunga MWENYEKITI mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amewasili Igunga jana jioni kwa ajili ya kufungua kampeni za CCM za ubunge katika Jimbo la Igunga, zinazotarajiwa kufanyika Jumamosi hii. “Nimewasili Igunga, wana-Igunga kazi ni moja, ni ushindi tu, alisema Mkapa akisalimia wananchi baada ya kupokewa katika kijiji cha Makomero kilometa nane kutoka …

Twiga Stars, Banyana Banyama watoka 2-2

TIMU ya Taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imetoka sare ya mabao 2-2 na Afrika Kusini (Banyana Banyana) katika mechi ya michezo ya All Africa Games (AAG) iliyochezwa leo Uwanja wa Machava jijini Maputo, Msumbiji. Banyana Banyana ndiyo iliyoanza kupata bao kabla ya Twiga Stars kusawazisha dakika ya 25 kupitia kwa Mwanahamisi Shuruwa. Banyana Banyana ilianza kipindi cha pili …

Serikali yaruhusu uwanja wa Taifa kutumika Ligi Kuu Vodacom

SERIKALI imeruhusu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinazohusu timu za Simba na Yanga. Hata hivyo ruhusa hiyo ni ya mechi mbili kwa wiki. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za VPL zenye maskani yake Dar es Salaam waliwasilisha tena maombi Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo …

JK apokea hati za mabalozi

Na Mwandishi Wetu RAIS Jakaya Kikwete leo asubuhi amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wa Australia, Finland, Mexico na Misri. Mabalozi Geoffrey Peter Tooth wa Australia na Balozi Luis Javier Campuzano wa Mexico watakuwa na makazi yao jijini Nairobi wakati Balozi Sinikka Antila wa Finland na Hossam Eldin Moharam wa Misri watakuwa na makazi yao hapa jijini Dar es …