RAIS wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete leo ameshiriki katika dua ya pamoja kuwaombea marehemu waliofariki dunia katika ajali ya Meli ya Mv. Spice Islanders iliyotokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita. Rais Kikwete katika dua hiyo ameungana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi na wananchi wa Zanzibar. Zifuatazo ni picha kuonesha dua ya pamoja.
Waokoaji kutoka Afrika Kusini wawasili Tanzania
Na Mohammed Mhina, wa Polisi Zanzibar WAPIGAMBIZI 12 toka nchini Afrika ya Kusini, wamewasili usiku wa kuamkia leo mjini Zanzibar kuungana na wazamiaji wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini kufanya uhakiki wa kujua kama bado kuna miili iliyonasa kwenye Meli ya Mv. Spice Islander iliyozama chini ya bahari eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja usiku wa Jumamosi …
Pinda, Lowassa wawasili Zanzibar kutoa pole kwa Dk. Shein
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu ndogo Migombani na kumpa pole kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya Spice Islanders hapo juzi alfajiri. Waziri Pinda akiwa amefuatana na baadhi ya Mawaziri wa …
Legendary Footballers Okocha, Desailly, Song & Bwalya
LEGENDARY FOOTBALLERS OKOCHA, DESAILLY, SONG AND BWALYA STEP UP TO THE GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ 12th September, 2011 Dar Es Salaam Tanzania: The GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™, for all lovers of the GREATNESS™ of Guinness® and the GREATNESS™ of Football, is here. This time around, the not-to-be-missed TV game show phenomenon is going to be even bigger and better than before as …
Simba, Yanga sasa kukipiga Chamazi
TIMU za Simba na Yanga sasa zitaanza kuutumia Uwanja wa Azam Chamazi ulioko Mbande, Dar es Salaam wiki hii. Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema, Septemba 14 mwaka huu Simba itakuwa mwenyeji wa Polisi Dodoma wakati siku inayofuata African Lyon itakuwa mwenyeji wa Yanga. Aliongeza kuwa viingilio kwa mechi zinazohusisha timu …