Nimepewa Mimba na ‘House Boy’; Je, Nimwambie Mumewangu?

NDUGU Mwandishi wa TheHabari, naomba utume hii post ili wasomaji wako waweze kunisaidia mawazo na ushauri.
Mimi naitwa Doroth, nimeolewa na Mume ninayempenda kwa miaka 4 sasa. Mume wangu anafanya kazi TRA na ana nafasi kubwa kazini.
Tatizo ni kwamba hatujajaliwa kupata mtoto. Mama mkwe na mawifi wameanza kunisimanga na kusema najaza choo cha ndugu yao bure, mawifi wanamshawishi kaka yao atafute mwanamke mwingine atakaye mzalia watoto.

Nimeshaenda kwa daktari akanipima na akasema sina tatizo lolote, nimejaribu kumbembeleza mume wangu aende kwa daktari ili kama naye ana matatizo aweze kutibiwa na amekataa.

Mume wangu alisafiki kikazi kwenda Mwanza kwa siku nne, na ‘weekend’ moja nilipitiwa nikalala na ‘house boy’ wetu na sijui niseme bahati mbaya au nzuri nimeshika mimba. Mpaka ninavyoandika mimba ina wiki 6.

Naombeni mnisaidie wasomaji wa Thehabari, Je nimwambie mume wangu kuwa nina mimba yake au nimwambie tu ukweli kwamba mimba sio yake na ni ya house boy wetu? Nampenda sana mume wangu na sitaki kumpoteza, najua tukipata huyu mtoto ndoa yetu itakuwa na amani sasa.

Asanteni sana kwa ushauri wenu.

Doroth.msichana-mzuri-macho-mazuri

Related Post

8 thoughts on “Nimepewa Mimba na ‘House Boy’; Je, Nimwambie Mumewangu?

  1. Umalaya umekuzidi mpaka unatembea na house boy, ulikuwa huna akili, ningekuwa mimi ningekupa adhabu kali ambayo usinge isahau milele.

  2. ni hatari lakini Salama’
    binafsi sijui saana nini cha kukushauri lakini kwanza la msingi angali mwenzi wako yuko vipi na kama unaona ni mtu wa kuridhika mueleze kwa namna ambayo wewe unaona haita leta mtafaruku zaidi kwa ule mtazamo uluosema unampenda mume wako na hautaki kumpoteza.

  3. Inasikitisha kuwa unalala hata na Houseboy.
    Na je kupitiwa maana yake ni nini?
    je Mumeo angekufanyia hilo?
    Kila kitu kina malipo na yako ndiyo hayo

  4. Kumbuka mumeo atahtaj mtoto zaidi ya mmoja. Je utamtafuta tena houseboy. La msingi ndoa ishayumba. Nakushaur jipange kimaisha kupitia mgogo wa mumeo kimyakimya. Kisha ukiona inaridhisha nenda nyumbn kwenu ukae na wazaz wako uwaeleze ukweli. Watamuita mumeo kuongea nae. Akishafaham uamuz utakuwa kwake ama kukusamehe au la.

Comments are closed.