Naomba Ndugu Zangu Wanisaidie kwa Ushauri…!


Hi Admin!, hide my name please, naomba
ndugu zangu wanisaidie kwa ushauri,
Mimi ni kijana mwenye miaka 27 ambaye
naishi Ubungo Kibangu,
mwaka huu Januari 9 ndio nilioa rasmi baada
ya kuchoka Maisha ya Ubachela,
Mke wangu huyu niliyevutiwa naye sasa kwa
haiba, tabia na hata mavazi yake, siku zote
tangu nakutana naye mara ya kwanza huwa
anavaa nguo ndefu na kujitanda mtandio, na
mimi kwa kuvutiwa zaidi nilimwambia
kamwe mtandio na nguo ndefu asiache na
akatii hilo, amekuwa mtiifu mpaka ndugu zangu
humsifia.
Tarehe 17 mwezi wa 4 mwaka 2013
ndipo yaliponikuta makubwa jamani, Mke
wangu aliniaga anaenda Morogoro
kuzungusha mzigo wa biashara yake ya
vitenge na atarudi baada ya siku 3, nikasema
ok,
Basi siku ya 2 mwenzenu nikajihisi upweke
basi usiku nikaenda zangu Bar moja maeneo
ya Mwenge kupata japo Castle bariiidi,
Wakati nimefika pale bar nikakuta kuna Show
ya kufa mtu ya Wale wanaoitwa “KANGA
MOKO!”
duh asikwambie mtu ile shoo ni laana aisee!
Nami mijicho ikanitoka kwa mfadhaiko
nikajikuta nasogea, duh kuna mdada alikuwa
anajibinua binua pale jukwaani
anashangiliwa huyo! Anavyokatika watu
wamepagawa! Aisee hata Mke wangu
hawezi!
Basi nikasogea nione Shoo vizuri, LAHAULA!!!
Kumbe ni Mke wangu jamani! Tena ule
mtandio anaovaaga kichwani leo upo
makalioni umeloweshwa maji!
Nimetoka nduki na mihasira mpaka Home,
nilipofika nikasubiri karibu masaa mawili
nikapiga simu, ajabu akapokea mwanaume
na kusema “hapa kibandani, simu ipo chaji”
dah roho haikutulia, kesho yake napiga
akapokea mwenyewe na kuniambia kwamba
bado Yupo moro salama kabisa Mpenzi
nisihofu,
NIMECHANGANYIKIWA JAMANI NISAIDIENI.

Related Post

3 thoughts on “Naomba Ndugu Zangu Wanisaidie kwa Ushauri…!

  1. UMEONAA BASI TATIZO LA KUTOOKOKA NDO HILO, KWA KWELI KAKA WEWE UNAMAKOSA MENGI TU TOKA MWANZO WAKO WA KUMPENDA HUYO DADA ULIKOSEA PALE ULIPO MWAMINI KIMAVAZI KWELI WEWE UNAMIJICHO NDO UNAPENDA PENDA, KITU CHA KUFANYA “MWAMBIE AKUPE TALAKA YAKO KISHA WEWE UAMUE KUMFUATA YESU KRISTO NA UKIRI KUWA NDIO CHANGUO LA MAISHA YAKO” BILA HIVYO HAUNA BAHATI MAISHANI RAFIKI YANGU . KWA USHAURI ZAIDI NI TAFUTE KWENYE WEBSITE YANGU “HEZZO DAKING”

  2. Kwanza una makosa kumpenda mwanamke kwa mavazi tu iliyompendeza na pili ulikuwa humjui hapo mwanzoni kama alikuwa chokoraa au mtu safi lakini ka jinsi alivyo huyo mwanamke alipokuambia anaenda kuzungusha biashara zake huko morogoro kwa muda wa siku 3 akili yako haikuchaji? Ni biashara ya aina gani imekosa soko hapa DAR mpaka ipelekwe morogoro? ndugu nasikitika sana hii itakuwa funzo kwako wanawake hawapewi ticket ya kutoka siku 3 na natumaini hutavutiwa na wakata njia tena na nimefurahi sana mungu amekuonyesha hakuwa mbali isipokua alikua mkata kiuno kwenye bar na unapomtaka mke angalia tabia na ujue ni mtu wa hali gani bila papara.

  3. Ndugu! Pole sana kwa hayo yaliyokukuta,hiyo ndiyo mitihani ya Mwenyezi Mungu.
    Tambua kuwa.jambo lolote linahusu mapenzi ni gumu sana kukufanyia maamuzi na mtu mwingine awe mzazi,ndugu,jamaa au rafiki.Kama ulivyoamua kumpenda wewe mwenyewe binafsi pasipo kuomba msaada kwa jamaa na ndugu,ndivyo maamuzi ya sasa uamue wewe mwenyewe kwa akili zako.
    USHAURI.
    Jipe moyo wa subira,japo ni ngumu sana.msubiri arudi nyumbani na kisha anza kumdodoso kidogo kidogo huku ukichukua tahadhari zote,upate ukweli toka kwake,kisha mpe ukweli na papo hapo fanya maamuzi.
    Poleeee!!!!!!!!!!

Comments are closed.