Lulu ‘Elizabeth’ afikishwa tena mahakamani

Lulu katikati (aliyevaa nguo nyekundu) akiwa katikati ya ulinzi wa askari wa Jeshi la Magerteza na Polisi leo alipofikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu
MSANII nyota wa filamu na chimpukizi, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la ‘Lulu’ leo amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kwa kesi ya tuhuma ya mauaji inayomkabili.

Lulu amefikishwa mahakamani hapo ikiwa ni mara ya pili tangu afunguliwe kesi hiyo, akituhumiwa kuhusika na kifo cha msanii nyota na maarufu marehemu Steven Kanumba. Kesi hiyo yenye mvuto kwa wengi leo tena ilikusanya umati mkubwa wa wananchi katika Mahakama ya Kisutu jambo ambalo liliwapa wakati mgumu askari magereza na polisi waliokuwa wakitoa ulinzi wa kesi hiyo.

Hata hivyo kesi hiyo imehairishwa tena kwa kile uchunguzi bado hujakamilika na inatarajiwa kutajwa tena Mai 7, 2012 katika mahakama hiyo. Tayari jopo la mawakili kadhaa wamejitokeza kumtetea Lulu katika mashtaka yanayomkabili kwa sasa.

Related Post

2 thoughts on “Lulu ‘Elizabeth’ afikishwa tena mahakamani

  1. Mimi katika moyo wangu jamani naona Lulu siye mtu aliye muuwa Kanumba, ila ni siku yake tu ilifika ya kufa. Hivyo nashauri aachiwe huru na kurudi nyumbani, kama atafungwa Kanumba tayari amekwenda na hawezi kurudi tena, la muhimu ni kuachiwa huru tu Lulu. Asante sana.

  2. Jamani Mr. Kanumba wakati wake ulifika kwani waswahili wanasema ajali haina kinga na kama halikuandikwa na muumba kamwe mwanadamu hatoliweza, ilipangwa Kanumba aondoke hivyo Lulu ni sababu tu hata kama asingekuwepo Lulu angeondoka kwa njia yoyote ile kilichobaki ni kumuombea Lulu hiyo kesi iishe. Lulu mdogo wangu kwa uwezo wa Rabuka atakufanyia wepesi, Inshallah.

Comments are closed.