
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha gari maalum ya kuinulia mizigo huku akipata maelezo kutoka kwa Balozi wa China nchini Lu Youqinq alipotembelea kiwanda cha nguo cha Dahong Textile kinachojengwa mkoa wa Shinyanga.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Balozi wa China nchini Lu Youqinq kuhusu mipango ya China katika kuwekeza Tanzania.