JE, WATAKA KUWASAIDIA WATANZANIA WENZETU WALIYOATHIRIWA NA MAFURIKO YA JIJI LA DAR ES SALAAM?

Baadhi ya nyumba zikiwa kwenye maji huku wananchi wakijaribu kujinusuru na maafa hayo ya mafuriko yaliotokea Dar es Salaam.

Ungana na Tanzania Professionals Network (TPN) kufanya hivyo kwa kuwasaidia walioathirika na mvua DSM kipindi hiki cha Siku Kuu za mwisho wa mwaka.

Naomba nichukue fursa hii kuwaomba wote wenye nia ya kuchangia waliothirika na maafa haya basi wawasiliane na TPN Staff Miss. Anna Machanga machangaanna@yahoo.com, 0652 945422; na Bw. ASED KIPEPE: sdkipepe@gmail.com, 0716 898685. Michango inayopokelewa ni fedha taslimu au hundi, vifaa vya nyumbani, vyakula, vinywaji, nguo mpya na zilizotumika n.k.

Kuchangia kwa M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na vinginevyo; wasiliana na Bw. Gervas Lufingo +255 (0784/0767/0658) 48 25 97 : nasemaasante@yahoo.com

Wafanyakazi hao wa TPN watakufuata ulipo na kupokea mchango wako na kukabidhi risiti. Michango yote itakayopatikana itawekwa hadhani na itawasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa DSM, Mhe. Mecky Sadik kwa ajili ya kufikishwa kwa waathirika. Kutoa ni Moyo na wala si utajiri.

Nachukua fursa hii kuwatakia wote siku kuu njema ya Krismas kwa wale wanaosherehekea, mapumziko mema ya mwisho wa mwaka na pia nawatakia wote mwaka mpya mwema na wenye mafanikio tele.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Mungu awabariki wote.

Phares Magesa, Rais- TPN
(www.tpntz.org)

Related Post

One thought on “JE, WATAKA KUWASAIDIA WATANZANIA WENZETU WALIYOATHIRIWA NA MAFURIKO YA JIJI LA DAR ES SALAAM?

  1. We offer loan at low Interest rate and with not
    credit check, we offer Personal loan, debt consolidation loan, venture
    capital, business loan, Education Loan, home loan OR “loan for any reason!.”

    Note: Any interested Applicants should get back to us by email for further
    information on Our loan program.

    Email: david.mutukufinance60@yahoo.com
    Mr.Mr David Mutuku.
    Thanks for your understanding to your contact as we Await.

Comments are closed.