






KAMPUNI ya Jamii Media wamiliki wa mitandao maarufu ya mijadala kwa jamii kupitia mitandao ya jamii, JamiiForums na Fikra Pevu nchini Tanzania imevuta watazamaji wengi kutembelea banda lao lililoshiriki katika Maonesho ya Biashara ya Bidhaa za Uturuki na Tanzania yaliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Wananchi wengi waliotembelea katika maonesho hayo walikuwa wakipita katika banda la Jamii Media na kupata maelezo juu ya namna mitandao hiyo inavyofanya kazi na ilivyo na manufaa kwa watumiaji (jamii kwa ujumla).
