Beki wa timu ya Mshindo, Anifa Kalinga (kulia), akimtoka mshambuliaji wa timu ya Nianjema, Zainab Maulid wakati wa Tamasha la Soka la kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani 2014, lililoandaliwa na IDYDC na Grassrootsoccer kwa udhamini wa ExxonMobil katika Uwanja wa Kituo cha Soka la
Matumaini cha FIFA, mjini Iringa jana. Tamasha hilo lilihusisha wachezaji 80 vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15 – 18 kutoka timu nane. Mshindo
ilishinda kwa bao 2-1. |