Mashabiki wa CCM wakimbeba mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini Godfrey Mgimwa, baada ya kupata matokeo ya awali na CCM kuongoza katika kata 11 kati ya 13 katika matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana. Shamrashamra hizo zilifanyika Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa.Mashabiki wa CCM wakishangilia kwa furaha baada ya kupata matokeo ya awali na CCM kuonekana kuongoza katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa.Mashabiki wa CCM wakishangilia kwa furaha baada ya kupata matokeo ya awali na CCM kuonekana kuongoza.
MATOKEO YA AWALI Yanaonesha kama Ifuatavyo:-
Mpaka sasa CCM inaongoza katika kata 11 kati ya 13
TOSA no.1 CCM 98, Chadema 20, CHAUSTA 0
Wasa CCM 149, Chadema 15 CHAUSTA 0
Usengelidete CCM 260, Chadema 46, CHAUSTA O
Chanzo:- theNkoromo Blog
Picha za Matukio ya awali Jimboni. Polisi akilinda moja vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi
Wazee wenye matatizo maalum wakisubiri kuitwa kupiga kura kwenye kituo cha Mangalale A, jimbo la Kalenga, wakati wa uchaguzi huo Msimamizi wa kituo cha kupigia kura cha Kalenga B, akimtafutia jina, Joseph Mdibule kwa ajili ya kupiga kura kwenye kituo hicho Wananchi wakiwa kwenye kituo cha kupiga kura cha Kalenga A wakati wa upigaji kura, katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini.