Wajasiriamali Tanga watakiwa kuungana

Na Mwandishi Wetu, Tanga WAJASIRIAMALI mkoani Tanga wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) ili kufanikisha lengo la kuunganisha nguvu za wajasiriamali na hatimae kujikwamua na umasikini. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Ndibalema Kisheru katika uzinduzi wa shughuli za wadau wa habari wa mradi wa MUVI mkoani hapa. …

Diwani amkana DC mkutanoni

Na Mwandishi Wetu, Ludewa DIWANI wa Kata ya Ludewa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Monica Mchiro, amemkana hadharani Mkuu wa Wilaya hiyo, Georgina Bundala. Sakata hilo limetokea mjini Ludewa baada ya mkuu huyo kushindwa kuweka bayana kilichotokea kati ya wananchi na watafiti wa madini walioanza shughuli katika ardhi ya Kata ya Iwela bila taarifa …

Kijiji cha Mahongole Njombe kujengewa Soko

Na Mwandishi Wetu, Njombe WAKULIMA wa nyanya katika Kijiji cha Mahongole kilichopo mkoa mpya wa Njombe wameahidiwa kujengewa soko na mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI), ili kuwaondolea kero ya kusafiri umbali mrefu kutafuta masoko. Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa Mradi huo mkoani hapa, Ofisa Mradi, Christopher Mkondya, amesema soko hilo ambalo kwa kiasi kikubwa litagharamiwa na mradi huo …

NMB kutoa mikopo kwa wajasiriamali

Na Mwandishi Wetu, Iringa MUUNGANO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) umefanikiwa kuwaunganisha wajasiriamali mkoani Iringa na Benki ya NMB mkoani humo, ili kuwasaidia kujipatia mafaniko zaidi katika kilimo. Akizungumza na wajasiriamali hao, Mratibu wa MUVI mkoa huo, Wilma Mwaikambo Mtui (pichani juu), amesema changamoto kubwa inayowakabili wakulima wengi ni upatikanaji wa mbegu pamoja na pembejeo za kilimo, hivyo kitendo cha kuwanganisha …

Bidhaa mbalimbali zitokanazo na zao la mhogo

Maandalizi ya awali ya zao la mhogo kabla ya kutumika kutoa bidhaa anuai za chakula. Miongoni mwa bidhaa zitokanazo na mhogo-hizi ni biskuti na tambi. Pichani ni Bi. Asumpta Mihanjo wa Songea akiwa ameshika kifaa kinachotengeneza bidhaa hizo. Mkurugenzi wa kikundi cha Iman (Imani group) akinadi bidhaa mbalimbali zinazo tokana na zao la mhogo ambazo zinatengenezwa na kikundi hicho, kikundi …

Wanajeshi wadaiwa kuvamia kijiji Dar

TAARIFA zilizotufikia jana majira ya saa nne asubuhi kutoka nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ni kwamba; watu wanaodaiwa kuwa ni Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi nchini (JWTZ) wamevamia Kijiji cha Kimbiji. Taarifa zinasema wanajeshi hao walivamia na kuvunjiwa makazi yao pamoja na kuharibiwa mazao. Chanzo cha habari cha mtandao huu kilisema, malori manne yaliyojaa wanajeshi yalikivamia Kijiji …