Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuanza kwa ligi ndogo Mei 11, 2016 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam itakayozishirikisha jumla ya timu nne. Timu zilishoshika nafasi ya pili katika msimamo wa SDL kwa kila kundi, Abajalo FC (Dar es salaam), Pamba FC (Mwanza), Mvuvumwa (Kigoma), Mighty Elephant (Songea) zitacheza ligi hiyo …
Mamadou Sakho Achunguzwa na UEFA
Beki wa Liverpool Mamadou Sakho anachunguzwa na UEFA kwa kufeli ukaguzi wa madawa ya kulevya. Ijapokuwa raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 hajapigwa marufuku rasmi, hatashiriki mechi yoyote wakati uchunguzi huo unapoendelea kulingana na Liverpool. BBC radio 5 inasema kuwa Sakho alipatikana na dawa za kusisimua misuli baada ya mechi ya UEFA kati ya Liverpool dhidi ya …
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kuanza Mei 14
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza Mei 14, 2016 kuwa tarehe ya kuanza kwa Ligi ya Mabingwa wa mikoa (RCL) itakayozishirkisha bingwa wa kila mkoa kutoka katika mikoa 27 nchini. Ligi hiyo ya mabingwa wa mikoa itachezwa katika vituo vine nchini, ambapo mshindi wa kila kundi atapanda moja kwa moja ligi daraja la pili (SDL) na mshindi wa …
Soma Hapa Matokeo ya Ligi Kuu ya Uingereza
Manchester City imepanda hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ya Uingereza baada ya kuicharaza Stoke City 4-0 huku ikitarajiwa kumenyana na Real Madrid katika ligi ya Mabingwa Ulaya siku ya Jumanne. Fernando alifunga kwa kichwa na kuwaweka City kifua mbele kabla ya Sergio Aguerro kufunga kwa njia ya Penalti. Baadaye Kelechi Ihienacho aliyetangazwa mchezaji bora katika mechi hiyo …
Kufa Kufaana Mbao Fc Yapanda Ligi Kuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitangaza klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao kutoka katika kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza chini (StarTimes League). TFF imeitangaza Mbao FC kfuatia maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF yaliyotolewa April, 2016 ya kuzishusha daraja timu nne kutoka kundi C baada ya …
DC Temeke Azinduwa Michuano ya UMISETA Dar
Wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye uzinduzi huo. Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Shule ya Sekondari ya Azania vilivyotolewa na Kampuni ya Coca Cola. Kulia Ofisa kutoka kampuni ya Coca Cola wadhamini wakubwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016. DC Mjema akisalimiana na mwamuzi …